MAZOEZI SI HAKIKA YA AFYA NJEMA

By Maureen C. Minanago Mazoezi ni muhimu kwa kukuweka mwenye nguvu muda wote lakini maisha unavyoyaishi pia yanachangia katika kukufanya mwenye furaha, mchangamfu na mwenye afya njema. Dr. Denis Nturibi anasema kuna vitu vitatu ambavyo binadamu wote tunapaswa kuvifuata ili kuwa na afya njema. Mazoezi ni sahihi kuyafanya lakini muundo wa maisha (lifestyle) yetu unamchango mkubwa pia. 1. Kula sahihi. Tunapaswa kupata lishe bora kwa maana kwamba tuachane na vyakula ambavyo vinanenepesha hasa vyenye mafuta mengi na sukari nyingi. Tusile sana yaani tule kwa kiwango na kwa muda tu. Kuna watu wanakula kwa siku hata zaidi ya mara nne. Kila unachoona unataka uonje. Basi tujitahidi kujiwekea mipaka yaani nini kiliwe na kwa muda na kiwango gani, Bila kusahau maji ya kunywa (angalau lita moja kwa siku). 2. Pumzika na lala. Tunafanya kazi kupata hela, sawa kabisa. Hata Mungu anatuambia tufanye kazi na ametuweka duniani hasa kufanya kazi bila hivyo hatupati kula. Lakini kila kitu kiwe kwa kiasi. Pata muda wa kutosha wa kupumzika. Kazi nyingi zinatufanya tutumie akili sana katika kufikiria, kusuluhisha na kudadavua mambo kitu ambacho huchosha sana akili na mwili pia.  Lala masaa yanayotakiwa (8-10). Usitumie muda mwingi kuangalia luninga ukakesha asubuhi unaelekea darasani au ofisini. Usisome masaa tisa ukalala kwa saa moja au kuvusha kabisa halafu uingie kufanya mtihani. Pumzika  na lala ili akili pia ipumzike na mwili kwa ujumla. 3. Shughuli za kimwili. Mazoezi ya viungo ni muhimu katika kukufanya mwepesi. Kimbia taratibu (jogging) au tembea kwa mwendo wa haraka kwa umbali kidogo kila siku au walau mara mbili kwa wiki. Hii itakusaidia kukupa pumzi nzuri. Kwa wale waimbaji, sauti yako itapunguza kuhema hema.Kwahiyo, Dr. Dennis anaeleza vizuri kuwa, mazoezi pekee si afya, lishe na kupumzika pamoja na kulala vinasaidia kwa afya bora. Unaweza kuwa na mwili mdogo na wenye nguvu sababu ya mazoezi lakini kama unakunywa pombe sana au unavuta sigara utakuwa na nguvu bila afya njema.Jitengenezee mazingira mzuri ya kuwa na afya muda wote kwani afya njema ndio kila kitu.

MAZOEZI SI HAKIKA YA AFYA NJEMA Read Post »

Tumbo la kuhara

By Maureen C. Minanago HUDUMA YA KWANZA Ni matumaini yangu hakuna mtu ambaye hajawahi kuumwa tumbo hata siku moja toka azaliwe. Lakini leo naongelea kuvurugwa kwa tumbo. Yawezekana ukawa umepata chakula mchnaganyiko ama vinywaji tofauti ambavyo vikasababisha kuvurugika kwa tumbo. Inawezekana ukawa umetoka sehemu moja kwenda nyingine yaani kubadilika kwa mazingira, hivyo kuhisi umevurugika tumbo. Lakini pia yawezekana ukawa unahofu sana kutokana na kusubiri matokeo fulani kama ya mtihani kimasomo ama majibu ya daktari ama ya usaili wa kazi. Yote haya na mengine mengi husababisha kuvurugika kwa tumbo na mara nyingi kupelekea kutaka kuhara (kuharisha). Mvurugiko huu wa tumbo humfanya mtu kukosa raha na hasa pale anapokuwa nje ya mazingira ya nyumbani ama sehemu iliyo karibu na huduma ya choo. Unachoweza kufanya ni kutafuta dawa ya kuzuia kuharisha kwenye maduka ya dawa yaliyoko karibu na wewe. LAKINI, si mara zote itawezekana kuwa hivyo, basi nini kifanyike unapokosa dawa hizo? Ukiwa nyumbani, chukua sukari na chumvi kisha chota chumvi kijiko kidogo cha chai nusu uweke kwenye kikombe na kiasi hicho hicho chota sukari uweke. Baada ya hapo changanya na maji kidogo sana ili kuepuka kupoteza ladha ya ukali dawa hiyo. Kwa kuwa uliweka kijiko kidogo nusu basi maji yaweke kiwango cha vijiko vikubwa vya kulia chakula vitano au sita. Koroga mchanganyiko wa chumvi na sukari kisha kunywa yote bila kuisikilizia. Tumbo litakata maumivu na dalili za kuhara mara moja. Na kama uliishaanza kuhara basi hali hiyo itaisha. Ukiwa nje ya mazingira ya nyumbani na hujapata msaada wowote wa chumvi na sukari ama dawa, basi tafuta maji safi ya kunywa walau lita moja kisha vuta pumzi ndani na nje kwa nguvu kwa muda wa dakika tatu mpaka tano. 

Tumbo la kuhara Read Post »

Feasting to Fishing

By Justin Mwita David “A Mindset transformation journey for African youth, shifting from Dependency to Self-Sufficiency” Africa has the youngest population in the world, with over 400 million young people aged between 15 to 35 years. This demographic presents both challenges and opportunities.  The majority of African youth are caught in a dilemma that is both complex and disheartening. They are perceived to be more interested in exploiting a flawed system for personal gain rather than aspiring to build a better society. This perception is based on the metaphorical observation that they chase after those who distribute fish, indicating a preference for immediate gratification (Feasting), and turn their backs on those who want to teach them how to fish (Fishing), symbolizing a disregard for long-term self-sufficiency and societal improvement. The allure of immediate gratification, represented by the distribution of fish, is a powerful force for many young Africans. On the other hand, the disregard for long-term self-sufficiency, symbolized by turning their backs on learning how to fish, reflects a lack of interest in acquiring skills and knowledge that could lead to sustainable success and societal contribution. This mindset has significant implications for society. It perpetuates a cycle of dependency and short-term thinking that hinders societal progress and development. Empowering African youth to transition from dependency to self-sufficiency is a task that requires the collective efforts of various stakeholders and the key to unlocking the full potential of the continent’s young population lies in several areas. African youth aspirations often do not align with the current and projected labor market demands in the region. Despite this, they are increasingly taking an active role in shaping their future, disrupting traditional views of African agriculture, industry, IT, and sustainability. By investing in education, skills development, entrepreneurship, civic engagement, and supportive ecosystems, we can unlock the full potential of the continent’s young population. It is time to shift the narrative from one of dependency to one of empowerment, where African youth are equipped with the tools and opportunities to build a brighter future for themselves and their communities. Regardless of whether you’re an educator, policy maker, parent, or a young individual, your viewpoint is invaluable. Let’s perpetuate this dialogue and collaborate to empower Africa’s youth. The actions we take today have the potential to sculpt the continent’s future. It is our deepest commitment at MBS Trinity care to ensure that we are leading in the journey of mindset transformation for the African youth and foster the spirit of growth and sustainability for a brighter future.

Feasting to Fishing Read Post »

EMPOWERING SECONDARY SCHOOL GIRLS IN DODOMA REGION THROUGH SANITARY PAD DISTRIBUTION

By Happiness Silivester Masatu Empowering secondary school girls in Dodoma Region through sanitary pad distribution is a crucial initiative aimed at addressing menstrual hygiene management (MHM) challenges and promoting girls’ education. Menstrual hygiene remains a significant barrier to girls’ education in many parts of the world, including Dodoma Region, where access to sanitary pads is limited, leading to absenteeism and dropouts among girls. This proposal outlines a comprehensive plan to distribute sanitary pads to secondary school girls in Dodoma Region, thereby empowering them to stay in school and pursue their education. Various initiatives have been implemented by governmental bodies and other relevant stakeholders, such as the Campaign for Female Education (CAMFED), African Medical and Research Foundation (AMREF), Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Population Services International (PSI), and FEMINA, to enhancing menstrual hygiene management for girl students in Tanzania. These programs encompass activities such as raising awareness among female students regarding the management of menstrual hygiene, delivering reproductive health education, and supplying sanitary pads to adolescent females. Despite the implementation of many efforts, Tanzania exhibits a subpar performance in terms of knowledge, attitude, and behavior regarding menstrual hygiene management, with discernible disparities observed between rural and urban regions. This is due to insufficient provision of hygiene products, access to clean water, sanitation facilities, and particularly within educational institutions, which have a detrimental effect on the management of menstruation among adolescent girls. Conduct Needs Assessment of six Schools in Dodoma region: Begin with a comprehensive needs assessment to understand the specific challenges faced by girls regarding menstrual hygiene management in Dodoma Region. Below is a table of findings from a research done in year 2023. Proposal : Empowering Secondary School Girls in Dodoma Region Through Sanitary  Pad Distribution               Result Areas Unit # Unit  Unit Rate Unit # Unit  Amount (TZS) Activity 1.1 Conduct  a comprehensive needs assessment to understand the specific challenges faced by girls regarding menstrual hygiene management in Dodoma Region ParticipantsAllowance  Pts           5   100,000.00 days 6                    3,000,000.00 Meals and refreshments  Pts           5     20,000.00 days 6                      600,000.00 Stationaries  Pts         10       4,000.00 days 6                      240,000.00 Contigency  Pts           1   500,000.00 days 1                      500,000.00 Car Hire  Pts           1   300,000.00 days 6                    1,800,000.00 Sub total                              6,140,000.00                  Activity 2.1 Distribution of Sanitary Pads to selected Secondary School in Dodoma region Procurement of Sanitary pads Pts   3,035            3,000     days      12                   109,260,000.00 Transport and logistics BOX       80            5,000     days        1                         400,000.00     Car Hire pts         1         300,000     days        6                       1,800,000.00     Hygene Education  workshop students         5         100,000     days        6                       3,000,000.00     Meals and refreshments Pst       10          30,000     days        6                       1,800,000.00    Contigency Pst         1         500,000     days        1                         500,000.00    Media people Pst         5          50,000     days        6                       1,500,000.00    Facilitation fee pts         1         200,000     days        6                       1,200,000.00   Photer & video pts         2         200,000     days        6                       2,400,000.00 Facilitation transport pts         1         100,000     days        6                         600,000.00 Subtotal                          122,460,000.00               Moniotoring and Evaluation:monitoring and evaluation framework to track the distribution process’s effectiveness and impact on girls’ attendance, academic performance, and overall well-being Participanta Allowance Pts           5   100,000.00 days 6                    3,000,000.00 Venue venue           1   200,000.00 days 2                      400,000.00 Stationery Pts         10       4,000.00 days 2                        80,000.00 Contogency Pts           1   500,000.00 days 1                      500,000.00         Car Hire Pts           1   300,000.00 days 6                    1,800,000.00 Sub-total                              5,780,000.00                                                                                                                                                                                                                                                                                     Sub total Monitoring Activities                          134,380,000.00               GRAND TOTAL                134,380,000.00 Hence, empowering secondary school girls in Dodoma Region through pad distribution is a vital step towards promoting gender equality in education and improving girls’ overall well-being. By providing access to sanitary pads and menstrual hygiene education, we can empower girls to stay in school, achieve their academic potential, and contribute positively to their communities. This proposal outlines a strategic plan to implement this initiative effectively, but its success depends on collaborative efforts and support from all stakeholders involved. Support girls, support mankind, at MBS we say, Kindness is the Greatest!

EMPOWERING SECONDARY SCHOOL GIRLS IN DODOMA REGION THROUGH SANITARY PAD DISTRIBUTION Read Post »

“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”.

By Maureen C. Minanago Kuna ulemavu wa aina mbali mbali. Machache yajulikanayo ni kushindwa kutembea kushindwa kutumia mikono, kutoona vizuri ama kutoona kabisa, ulimi kuwa mzito hivyo kushindwa kuongea, kutosikia (kiziwi), mifupa kujikunja na kusababisha matege pamoja na kukosa melanin itengenezayo rangi ya ngozi (albino). Watu wenye ulemavu wanapaswa kujijali pia, wanapaswa kupata lishe iliyo bora kabisa ili kujikinga na maradhi. Hawapaswi kujihurumia na kujitenga, bali kuwa na jamii yao, hivyo kuwa na afya ya mwili na akili na kuwa na amani. Dkt. Abdallah Possi ni mtu mwenye albinism lakini anatumia fursa ya kuwa kiongozi kuielimisha jamii zaidi juu ya watu wenye ulemavu na kuwaasa waachane na mitazamo potofu ya kulionea kundi hilo.  Dkt Possi anasema, ”Kila mtu ni sawa lakini usawa huo uzingatie mtu na mtu; yaani, kila mtu aheshimiwe na kusikilizwa kulingana na nafasi ama hali aliyonayo”. Kundi la watu wenye walemavu limeonekana kuachwa nyuma kwani ni wachache na watu wengi wameonekana kuwaacha walio wachache na wale wachache wanajiona sio wa kawaida.  Amesema, ili kutibu historia ya muda mrefu ya watu wenye ulemavu kuachwa nyuma, haipaswi kuwepo kwa mtazamo wa upendeleo bali wachangamke ili kujitoa katika kundi walilomo kama; ilivyokuwa katika swala la wanawake.

“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”. Read Post »

AFYA ni nini?

By Maureen C. Minanago Afya ni hali ya kutokuwa na ugonjwa au kidonda. Afya ni hali ya kuwa na amani ya roho. Afya ni ubora wa akili, mwili na nafsi. Afya hutegemea vitu hivi vitatu ili kuwa hai na salama: Akili, Mwili, Nafsi. Akili ni utashi tuliopewa na Mwenyezi Mungu katika kung’amua mambo ulimwenguni. Akili hujumuisha uelewa, ufikiri, uamuzi na utendaji wa mambo. Hakuna awezaye kutafsiri akili yetu ila matendo yetu yanaweza kumfanya mtu aone flani yuko vipi; nayo bado itakuwa mtazamo wake sababu tunatofautiana kufikiri pia.  Binadamu hutumia akili kila siku na kila wakati ili kuelewa, kufikiri, kuamua na kuhakikisha tunatimiza jambo. Kwa maana hiyo, tunapaswa kuipumzisha “PUMZISHA AKILI”. Akili ikichoka mwili nao huchoka na hutafanya chochote sababu haitakuwa na uwezo mzuri kutenda. Lala au oga au ogelea au sikiliza mziki au chochote ukipendacho ambacho hakitakufanya utumie nguvu ya akili. Mwili ni muundo wote wa binaadam. Ni maumbile ya mtu. Mwili huhusisha yote yaliyotengeneza “mtu” mfano viungo kama miguu, mikono n.k, Maji kama mate, damu n.k, na vingine kama mishipa kucha na nywele. Tunapaswa kujipenda kwa kula vizuri, kulala vizuri na pazuri, kuvaa vizuri na kujijali muda wote kwa kuuweka mwili salama mfano kwa kupiga mswaki baada ya kula, kuosha nywele mara kwa mara, kukata na kusafisha kucha, kuoga, na kuvaa nguo safi. Pia tujiepushe na hatari, ugomvi na makwazo kwa faida ya mioyo yetu.  Ukitembea sana juani pata kivuli unywe na maji. Penye baridi uvike mwili wako kwa sweta ama nguo nzito. Ukiumia au kuumwa pata matibabu sahihi kwa kwenda hospitalini. Jipende, Ujali mwili wako. Tukifanya hivyo miili yetu itakuwa salama.  Nafsi ni roho yenye kuleta imani ndani yetu. Sisi huamini vitu mbali mbali kwa msaada wa nafsi. Lakini yote heri kama tutaamini vitu vyenye kujenga na sio kubomoa. Nafsi pia hutofautiana ya mtu na mwingine ndio maana tukawa tofauti japo chimbuko letu kiuumbaji ni moja.  Nafsi nayo huhitaji utulivu ili kuupa mwili na akili nguvu za kuishi kwa afya. Pata muda wa kutulia ukiongea na WEWE kujua nini waweza fanya LAKINI, mshirikishe MUUMBA wako kwa yote kupata amani uitakayo moyoni na kwa wakuzungukao. Hivyo basi, jipe likizo au omba likizo. Tembelea sehemu mbali mbali za starehe au vivutio kutuliza mwili, akili na roho pia. Ongea vizuri na watu, cheka, tabasamu hata kama umeumizwa. Inasaidia sana.  Afya ya vitu vyote vitatu ni muhimu katika kukuweka mwenye nguvu na furaha.  Jali afya yako!

AFYA ni nini? Read Post »

Kazana

By Maureen C. Minanago Endelea kukimbia hata kama ni wa mwisho katika mashindano. Huwezi jua, yawezekama ukawa bingwa. Ninawakummbusha ndugu zanguni kutokata tamaa maana muda unaokata tamaa unaweza kuwa ndio muda sahihi kabisa kwa wewe kupata mafanikio/ ukitakacho/ ulichoomba kwa muda mrefu/ kufikia ndoto zako na kadhalika. Ukihisi kuacha usiache, kazana kwa kuwa umekaribia. Sote ni washindi kwa muda tofauti na kwa namna tofauti.

Kazana Read Post »

KUMBATO NI TIBA

By Maureen C. Minanago Kumbato mara nyingi hutumika tunaposalimiana ama kuagana kwa furaha na wapendwa wetu. Hii ni ishara ya furaha na mara nyingi huchukua sekunde chache sana kama 3 mpaka 6.  Tunaposalimiana kwa mikono tunakuwa na umbali kiasi flani na ndiyo maana tunapokuwa makazini ama tukikutana na watu kwa mara ya kwanza tunapeana mikono kwa kuwa hatujawa karibu kiasi cha kuonyesha hisia zetu hasa za furaha kwao. Kitendo cha kukumbatia ni sehemu mojawapo ya kudumisha upendo kati yetu na tuwapendao. Na kumbato hilo hilo hugeuka kuwa tiba hasa tunapotumia sekunde nyingi zaidi walau 20 na kuendelea. Unapomkumbatia mtu ipasavyo, unakuwa na nafasi kubwa sana ya kuondoa ugonjwa, kutuliza hasira, kutuliza au kuondoa shauku, kutoa upweke, kupoteza huzuni na hata kupunguza na kuondoa kabisa msongo wa mawazo. Tuangalie manufaa ya kumbato kwa undani wake: Malezi yanayohusisha mguso wa kumbato hujenga hali ya uaminifu na hisia ya usalama. Hii husaidia kuleta mawasiliano ya wazi na yenye uaminifu. Kumbato linaweza kuongeza kiwango cha Oxytocin papo hapo na kukuinulia hisia chanya. Nayo hutoa hisia ya upweke, kutengwa, shauku kali na hasira. Kukumbatia kwa muda mrefu hunyanyua viwango vya Serotonin hivyo kuinua mudi ya kujenga furaha. Kumbato huimarisha mfumo wa kinga hivyo kukulinda na magonjwa. Shinikizo la taratibu katika Sternum na chaji za hisia, hujenga na kufanya Solar Plexus Chakra kuwa hai hivyo kuchochea kongosho tezi, ambayo husimamia uzalishwaji wa seli nyeupe za damu mwilini. Solar Plexus Chakra ni msingi wa utu wetu, utambulisho wetu na u-sisi wetu.  Unapokumbatia unalegeza mishipa. Hii huondoa mvutano mwilini mwako na kukuondolea maumivu kwa kuongeza mzunguko katika tishu laini hivyo kukupoza na kukupa tulizo. Kumbato huweka usawa katika mfumo wa neva. Majibu ya mtu ya ngozi ya Galvanic katika kutoa na kupokea kumbato huonyesha mabadiliko ya nguvu katika ngozi. Athari ndani ya unyevu na umeme katika ngozi hupendekeza hali ya usawa zaidi katika mfumo wa neva. Ni jambo linalotufundisha kutoa na kupokea. Ukikumbatiana na mtu au watu unapata thamani ya usawa ya kutoa na kupokea joto kama kutoa na kugawana. Inaelimisha juu ya upendo kwa wote wakumbatianao (wawili, watatu au kundi). Kukumbatiana ni kama tafakari ya undani au kicheko cha furaha ambavyo kufdunza kusahau ama kupotezea yale yanayobugudhi, yanayokwaza au kuumiza na kujikita katika usasa yaani kuishi kwa wakati uliopo.  Kumbato hukufanya ujisikie uko hai. Hukupa mzunguko wa mawazo mbalimbali yaliyo katika maumbo tofauti na kukuunganisha na moyo pamoja na pumzi yako. Kumbato huletea hali ya kujiamini. Hali ambayo imekaa ndani yetu toka udogo wetu ambapo tumekuwa tukikumbatiwa na kubebwa kwa upendo na wapendwa wetu kama ndugu jamaa na marafiki. Hisia hizi zimekuwa ndani yetu kadiri tukuavyo hivyo kutujengea nguvu na uwezo wa kujipenda. Kumbato la nguvu linalogusisha mioyo ya wawili wakumbatianao hufanya upendo kati yao kuwa maradufu hivyo kuweka uzio usioweza kuwatenganisha kirahisi kwani upendo ni dawa ya ajabu.  Kumbato pia huimarisha saikolojia yetu na kuleta maendeleo ya miili yetu kwani hukufanya tulivu na mwenye afya ya roho na mwili pia. Nguvu unayobadilishana na umkumbatiaye huwekezwa katika mahusiano yenu (mama na mwana, baba na mwana, marafiki, kaka na dada, wapenzi na kadhalika). Nguvu hiyo huleta hamasa ya uelewa baina yenu na mwisho kuwafanya mdumu. Pia husaidia kunyoosha misuli ya nyuso, kuondoa mikunjo ya uzee pamoja na kufanya uzee uje taratibu ama kupunguza kasi ya uzee. Varginia Satir ni mtaalamu anayeheshimika katika mambo ya familia. Yeye aliweza kufanya utafiti mdogo na kujiwekea msemo ambao sote tukiuzingatia tunaweza imarisha afya zetu kwa kiwango fulani. Anasema: *Tunahitaji kumbato mara 4 kwa siku ili KUISHI * Tunahitaji kumbato mara 8 ili KUREKEBISHIKA / KUIMARIKA *Tunahitaji kumbato mara 12 ili KUKUA Kwa wale wapendanao (wapenzi), kumbato ni chanzo kikubwa cha kuboresha mahusiano yenu  na tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, wapenzi wanaokumbatiana sana hudumu kwenye mahusiano yao kwa muda mrefu. Tibu maumivu yako sasa, tibu upweke na hali zote mbaya unazozipata kwa kupata kumbato. Anza kukumbatia watu zaidi kwa tiba rahisi zaidi.

KUMBATO NI TIBA Read Post »

Moyo wa Binadamu

By Maureen C. Minanago Je, unaufahamu kuwa kila mwanadamu anapumua kwa msaada wa moyo? Na je, unafahamu kuwa moyo huo huo unaweza kumfanya mtu kuwa na furaha ama huzuni? Hii ni alama ambayo wengi huitumia kuashiria moyo na moyo huo basi unatumika kama ishara ya upendo. Moyo ni pampu inayosukuma damu kupitia mishipa ya damu. Kupitia mishipa hiyo damu husambazwa mwili mzima ili kukupatia hewa safi (oxygen). Tukiachana na maswala ya kibaiolojia, moyo unakazi ya kupenda. Basi tuone upendo huo unaathiri vipi moyo na wewe kama binadamu unaukosea vipi moyo wako ama moyo wa mwingine. Jijali, mjali na mwenzio ili kuufurahisha moyo kwa afya zaidi. Huu ni moyo wa binadamu. Unapokuwa umezungukwa na watu wakupendao haijalishi ni upendo wa aina gani, moyo huwa na nguvu na hufanya kazi yake vizuri. Kila mmoja anapenda kupendwa, hata wababe huwa na wafuasi wao hata kama hawana upendo wa dhati. Moyo wenye furaha. Moyo wenye nguvu… Moyo wenye furaha huimba ndani yetu pale tunapoongeza marafiki wapya. Moyo wenye furaha huupoza mwili tusikiapo baridi yaani tuwapo wapweke, kwa kukumbuka mema mengi yaliyopita. Inawezekana kabisa kwa wewe kujichangamsha bila kusubiri kuchangamshwa. Moyo imara ni moyo wenye nguvu kwani unaweza kupigana na majaribu yote yanayotukumba katika maisha. Sisi sote tunapaswa kuwa na moyo wenye nguvu kwani pia ni rahisi kupingana na magonjwa tukianza na ugonjwa wa ‘moyo’ wenyewe. Upendo wa nguvu Upendo wa mahusiano ya kimapenzi ni upendo unaoleta hisia za kipekee. Kila mmoja anaweza kuuelezea ajuavyo yeye. LAKINI, maumivu ya kuachana kwa wapenzi hao yanaweza kuwa yanafanana kwani yote huumiza moyo. Upendo unaolega lega Afya ya mtu ni ya thamani, ni vema kutumia nafasi unayopata kwa mpenzi wako kumuonesha upendo na kupata upendo kutoka kwake. Kama unadhani hujaamua bado kujiingiza kwenye mahusiano, basi tafakari kabla ya kuchukua hatua. Ni vema kujiamini kwa ulifanyalo kuepukana na maumivu ya moyo. Kipindi tu unapojihusisha na mahusiano ya kimapenzi, fahamu kuwa unajifunga. Moyo uliofungwa kwa upendaye, usiufungulie kwa wengine. Angalizo: Ili kuulinda moyo (wako/mwemzako) na maumivu zingatia haya:- Ukipata mwenzako mshikilie sawa sawa. Ni bora kuumia kidole kitapona au kuvunjika kidole vingine vitafanya kazi lakini sio kuumia moyo sababu maumivu yake yaweza kuchukua miaka kuisha na kuvunjika kwa moyo ni ngumu kuutengeneza ukafanya kazi sawia. Kuna Moyo usioweza kufanya maamuzi sahihi, Moyo ulionyong’onyea na kudhoofika na Moyo uliochanganyikiwa. Hapa ndipo tunaposhauriwa kuwa na imani kwa kumuomba Mungu kwani yeye ndiye aliyekupa maisha. Jijali kwa kuepukana na athari hizo lakini pia, kama ikitokea ushaumizwa basi jitahidi kujishughulisha sana ili kupunguza mawazo. Kaa na watu watakupa mawazo tofauti usikae mwenyewe ukiwa mpweke kuepukana na mawazo potofu. Kemea roho ndani yako inayokusukuma kukata tamaa, kuchukia ama kujiua. Sali sana ukisikia hivyo kwa afya ya Roho na moyo pia. Maumivu makali ya moyo Usiuzeeshe moyo wako kwa mambo usiyoyaweza. Usiukondeshe kwa kuupa mambo mengi usiyoweza kuyafuatilia na kuyafanya kwa ufanisi, usiufanye ukaelemewa. Ujali moyo wako kwa kujipenda na kuwa makini. Lakini kikubwa, usiutegemee moyo pekee katika mapenzi, shirikisha akili yako. Ni kwa kufanya hivyo, moyo utabaki kupenda tu huku mengine yakifanywa kwa utashi uliobarikiwa nao.

Moyo wa Binadamu Read Post »

Scroll to Top