By Sylvia Mtenga

Katika falsafa za kisasa za kiroho na maendeleo binafsi, manifestation ama udhihirisho unahusishwa na nadharia kwamba mawazo yetu yana nguvu ya kuathiri hali halisi. Hii inamaanisha kwamba kile tunachokifikiria na kukihisi mara nyingi kinaweza kugeuka kuwa uhalisia wetu. Ikiwa unalenga kwenye fikra chanya na kujenga picha nzuri kuhusu maisha yako, unaweza kuvutia hali hizo chanya kwenye maisha yako.
Hii inamaana kwamba mawazo na maneno yetu yana nguvu ya kusababisha mambo kutokea ama kufanyika, hivyo ni jambo la msingi sana kama tukitilia maanani mambo tunayoyatamka ama kuyawaza. Msemo wa maneo huumba haukukosewa.

Tujifunze kujinenea maneno mazuri na tutazame jinsi Maisha yetu yanavyo badilika na tunakua wenye furaha na utulivu.
Kwa kuanza, hapo chini nimekuwekea maneno tisa unayoweza kujiambia kila siku, ili kuhakikisha yanakaa katika kumbukumbu za kudumu na kufanya Maisha yako kua na hisia chanya
MANENO HAYO NI HAYA
- Ninauwezo
- Ninajiamini
- Nimefanikiwa
- Ninapendwa
- Ninatosha
- Niko salama
- Ninafuraha
- Niko pale ninapopaswa kuwa
- Ninaamini katika uwezo wangu
