Hofu ya kuzungumza

By Maureen C. Minanago Hofu ya mwanadamu hutofautiana kwa ukuu. Lakini sote huogopa kwa namna fulani. Hata mwenye nguvu wanamaeneo yao ya unyonge. Tuogope yote lakini tusiogope kusema ukweli inapobidi, na si ukweli tu ila kuzungumza kwa ujumla. Wapo wenye mawazo mazuri sana ambayo yasipokaliwa kimya yanaweza kuleta athari kubwa tu kwa mtu mmoja au jamii nzima.Yamkini ukambadilisha mtu / watu, ukaokoa maisha ya mtu / watu, ukapata msaada ulioukusudia au kuutamani kwa muda mrefu, ukatambulika katika familia, ukoo, eneo, nchi, bara au dunia kwa kusema kwako. Usisite, usikate tamaa, usiogope kusema sababu yule ni mtu mzima, yule ni mkali, yule ni mpole sana, yule haeleweki, yule simuamini. Usihisi labda hivi, labda vile. Sema usikike hata kama utamkwaza, hata kama utamuudhi, hata kama atakujibu vibaya, atakukaripia, atakutukana ama atakukalia kimya. Katika yote, hakika kuna ambalo litamgusa na kumbadilisha japo kidogo. Kama ni cha thamani kiseme…kitaleta mabadiliko!! Kiseme, moyo wako uridhike pia!! Katika sehemu ya tatu, kifungu cha 18 cha Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, tunaona kuwa kila mwanadamu anauhuru wa kuongea / kuzungumza. Kumbe basi, ni wajibu wa kila mmoja kuzungumza kile anachoona ni sahihi, ilimradi tu asiseme uongo wala kuzusha jambo. Usiogope!!

Hofu ya kuzungumza Read Post »

Kila lililokamilika huanza kwa uamuzi wa kujaribu.

By Maureen C. Minanago Msemo wa leo ni wa kutuhamasisha zaidi juu ya uthubutu. Chukua mfano huu mdogo. Umekaa kochini ukatamani maji ya kunywa lakini unaona uvivu kunyanyuka, hutapata maji. Kuna watu ndani unashindwa kuwaomba msaada wakuletee, hutapata maji. Umepata ila ni ya moto unahitaji ya baridi na huchukui uamuzi wowote, hutakata kiu yako. Sasa, unataka kufanikisha mipango yako ambayo pengine hujaanza hata kujipanga, hutaikamilisha. Inatakiwa ifikie wakati ambapo utasimama hata kama umechoka au hujiwezi kufedha au kimwili. Anza safari huku ukiomuomba Mungu, naye atakuimarisha ukiwa njiani na utafika salama. Fanya maamuzi haraka ya wapi uanze ama wapi upite na sio maamuzi ya kuendelea kusubiri. Bora ujaribu ushindwe kuliko usijaribu kumbe unajikosesha faida. Na ukijaribu ukashindwa usikate tamaa haraka, jaribu tena na tena mpaka utakapoona haiwezekani kabisa; ingawaje hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Utachelewa lakini sio kushindwa. Kazi kwako… KUWA MTU MZURI LAKINI USIPOTEZE MUDA KUTHIBITISHA

Kila lililokamilika huanza kwa uamuzi wa kujaribu. Read Post »

EMPOWERING SECONDARY SCHOOL GIRLS IN DODOMA REGION THROUGH SANITARY PAD DISTRIBUTION

By Happiness Silivester Masatu Empowering secondary school girls in Dodoma Region through sanitary pad distribution is a crucial initiative aimed at addressing menstrual hygiene management (MHM) challenges and promoting girls’ education. Menstrual hygiene remains a significant barrier to girls’ education in many parts of the world, including Dodoma Region, where access to sanitary pads is limited, leading to absenteeism and dropouts among girls. This proposal outlines a comprehensive plan to distribute sanitary pads to secondary school girls in Dodoma Region, thereby empowering them to stay in school and pursue their education. Various initiatives have been implemented by governmental bodies and other relevant stakeholders, such as the Campaign for Female Education (CAMFED), African Medical and Research Foundation (AMREF), Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Population Services International (PSI), and FEMINA, to enhancing menstrual hygiene management for girl students in Tanzania. These programs encompass activities such as raising awareness among female students regarding the management of menstrual hygiene, delivering reproductive health education, and supplying sanitary pads to adolescent females. Despite the implementation of many efforts, Tanzania exhibits a subpar performance in terms of knowledge, attitude, and behavior regarding menstrual hygiene management, with discernible disparities observed between rural and urban regions. This is due to insufficient provision of hygiene products, access to clean water, sanitation facilities, and particularly within educational institutions, which have a detrimental effect on the management of menstruation among adolescent girls. Conduct Needs Assessment of six Schools in Dodoma region: Begin with a comprehensive needs assessment to understand the specific challenges faced by girls regarding menstrual hygiene management in Dodoma Region. Below is a table of findings from a research done in year 2023. Proposal : Empowering Secondary School Girls in Dodoma Region Through Sanitary  Pad Distribution               Result Areas Unit # Unit  Unit Rate Unit # Unit  Amount (TZS) Activity 1.1 Conduct  a comprehensive needs assessment to understand the specific challenges faced by girls regarding menstrual hygiene management in Dodoma Region ParticipantsAllowance  Pts           5   100,000.00 days 6                    3,000,000.00 Meals and refreshments  Pts           5     20,000.00 days 6                      600,000.00 Stationaries  Pts         10       4,000.00 days 6                      240,000.00 Contigency  Pts           1   500,000.00 days 1                      500,000.00 Car Hire  Pts           1   300,000.00 days 6                    1,800,000.00 Sub total                              6,140,000.00                  Activity 2.1 Distribution of Sanitary Pads to selected Secondary School in Dodoma region Procurement of Sanitary pads Pts   3,035            3,000     days      12                   109,260,000.00 Transport and logistics BOX       80            5,000     days        1                         400,000.00     Car Hire pts         1         300,000     days        6                       1,800,000.00     Hygene Education  workshop students         5         100,000     days        6                       3,000,000.00     Meals and refreshments Pst       10          30,000     days        6                       1,800,000.00    Contigency Pst         1         500,000     days        1                         500,000.00    Media people Pst         5          50,000     days        6                       1,500,000.00    Facilitation fee pts         1         200,000     days        6                       1,200,000.00   Photer & video pts         2         200,000     days        6                       2,400,000.00 Facilitation transport pts         1         100,000     days        6                         600,000.00 Subtotal                          122,460,000.00               Moniotoring and Evaluation:monitoring and evaluation framework to track the distribution process’s effectiveness and impact on girls’ attendance, academic performance, and overall well-being Participanta Allowance Pts           5   100,000.00 days 6                    3,000,000.00 Venue venue           1   200,000.00 days 2                      400,000.00 Stationery Pts         10       4,000.00 days 2                        80,000.00 Contogency Pts           1   500,000.00 days 1                      500,000.00         Car Hire Pts           1   300,000.00 days 6                    1,800,000.00 Sub-total                              5,780,000.00                                                                                                                                                                                                                                                                                     Sub total Monitoring Activities                          134,380,000.00               GRAND TOTAL                134,380,000.00 Hence, empowering secondary school girls in Dodoma Region through pad distribution is a vital step towards promoting gender equality in education and improving girls’ overall well-being. By providing access to sanitary pads and menstrual hygiene education, we can empower girls to stay in school, achieve their academic potential, and contribute positively to their communities. This proposal outlines a strategic plan to implement this initiative effectively, but its success depends on collaborative efforts and support from all stakeholders involved. Support girls, support mankind, at MBS we say, Kindness is the Greatest!

EMPOWERING SECONDARY SCHOOL GIRLS IN DODOMA REGION THROUGH SANITARY PAD DISTRIBUTION Read Post »

“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”.

By Maureen C. Minanago Kuna ulemavu wa aina mbali mbali. Machache yajulikanayo ni kushindwa kutembea kushindwa kutumia mikono, kutoona vizuri ama kutoona kabisa, ulimi kuwa mzito hivyo kushindwa kuongea, kutosikia (kiziwi), mifupa kujikunja na kusababisha matege pamoja na kukosa melanin itengenezayo rangi ya ngozi (albino). Watu wenye ulemavu wanapaswa kujijali pia, wanapaswa kupata lishe iliyo bora kabisa ili kujikinga na maradhi. Hawapaswi kujihurumia na kujitenga, bali kuwa na jamii yao, hivyo kuwa na afya ya mwili na akili na kuwa na amani. Dkt. Abdallah Possi ni mtu mwenye albinism lakini anatumia fursa ya kuwa kiongozi kuielimisha jamii zaidi juu ya watu wenye ulemavu na kuwaasa waachane na mitazamo potofu ya kulionea kundi hilo.  Dkt Possi anasema, ”Kila mtu ni sawa lakini usawa huo uzingatie mtu na mtu; yaani, kila mtu aheshimiwe na kusikilizwa kulingana na nafasi ama hali aliyonayo”. Kundi la watu wenye walemavu limeonekana kuachwa nyuma kwani ni wachache na watu wengi wameonekana kuwaacha walio wachache na wale wachache wanajiona sio wa kawaida.  Amesema, ili kutibu historia ya muda mrefu ya watu wenye ulemavu kuachwa nyuma, haipaswi kuwepo kwa mtazamo wa upendeleo bali wachangamke ili kujitoa katika kundi walilomo kama; ilivyokuwa katika swala la wanawake.

“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”. Read Post »

AFYA ni nini?

By Maureen C. Minanago Afya ni hali ya kutokuwa na ugonjwa au kidonda. Afya ni hali ya kuwa na amani ya roho. Afya ni ubora wa akili, mwili na nafsi. Afya hutegemea vitu hivi vitatu ili kuwa hai na salama: Akili, Mwili, Nafsi. Akili ni utashi tuliopewa na Mwenyezi Mungu katika kung’amua mambo ulimwenguni. Akili hujumuisha uelewa, ufikiri, uamuzi na utendaji wa mambo. Hakuna awezaye kutafsiri akili yetu ila matendo yetu yanaweza kumfanya mtu aone flani yuko vipi; nayo bado itakuwa mtazamo wake sababu tunatofautiana kufikiri pia.  Binadamu hutumia akili kila siku na kila wakati ili kuelewa, kufikiri, kuamua na kuhakikisha tunatimiza jambo. Kwa maana hiyo, tunapaswa kuipumzisha “PUMZISHA AKILI”. Akili ikichoka mwili nao huchoka na hutafanya chochote sababu haitakuwa na uwezo mzuri kutenda. Lala au oga au ogelea au sikiliza mziki au chochote ukipendacho ambacho hakitakufanya utumie nguvu ya akili. Mwili ni muundo wote wa binaadam. Ni maumbile ya mtu. Mwili huhusisha yote yaliyotengeneza “mtu” mfano viungo kama miguu, mikono n.k, Maji kama mate, damu n.k, na vingine kama mishipa kucha na nywele. Tunapaswa kujipenda kwa kula vizuri, kulala vizuri na pazuri, kuvaa vizuri na kujijali muda wote kwa kuuweka mwili salama mfano kwa kupiga mswaki baada ya kula, kuosha nywele mara kwa mara, kukata na kusafisha kucha, kuoga, na kuvaa nguo safi. Pia tujiepushe na hatari, ugomvi na makwazo kwa faida ya mioyo yetu.  Ukitembea sana juani pata kivuli unywe na maji. Penye baridi uvike mwili wako kwa sweta ama nguo nzito. Ukiumia au kuumwa pata matibabu sahihi kwa kwenda hospitalini. Jipende, Ujali mwili wako. Tukifanya hivyo miili yetu itakuwa salama.  Nafsi ni roho yenye kuleta imani ndani yetu. Sisi huamini vitu mbali mbali kwa msaada wa nafsi. Lakini yote heri kama tutaamini vitu vyenye kujenga na sio kubomoa. Nafsi pia hutofautiana ya mtu na mwingine ndio maana tukawa tofauti japo chimbuko letu kiuumbaji ni moja.  Nafsi nayo huhitaji utulivu ili kuupa mwili na akili nguvu za kuishi kwa afya. Pata muda wa kutulia ukiongea na WEWE kujua nini waweza fanya LAKINI, mshirikishe MUUMBA wako kwa yote kupata amani uitakayo moyoni na kwa wakuzungukao. Hivyo basi, jipe likizo au omba likizo. Tembelea sehemu mbali mbali za starehe au vivutio kutuliza mwili, akili na roho pia. Ongea vizuri na watu, cheka, tabasamu hata kama umeumizwa. Inasaidia sana.  Afya ya vitu vyote vitatu ni muhimu katika kukuweka mwenye nguvu na furaha.  Jali afya yako!

AFYA ni nini? Read Post »

Onyesha heshima hata kwa watu wasiostahili; sio kwa muonekano wa tabia zao ila muonekano wa yako.

By Maureen C. Minanago Maneno ya Dave Willis yanakumbushia utoaji wa heshima. Waswahili wanasema “heshima ni kitu cha bure” yaani huhitaji kulipia wala kugharamia chochote kuheshimu ama kuheshimiwa ila kujiheshimu na kutoa heshima hiyo kwa wengine wote hata kama hawastahili heshima yako. Inakuwaje mtu hastahili heshima yako? Ni kwa sababu haonyeshi upendo kwako kama binadamu, sababu anakuona uko chini sana, sababu anakudharau, anakuona hufai kwake na katika maisha yake, sababu huna uwezo kifedha ama kifikra, sababu huwezi kufika alipofika, sababu hujampa alichotaka, hauna muonekano mzuri na mengine mengi. Zipo sababu nyingi lakini pamoja na yote tunapaswa kukumbuka kuwa sote ni binadamu na tunakosea. Inawezekana tukapishana leo  lakini tukumbuke dunia huzunguka, binadamu pia. Tuheshimiane kwani hatujui ya kesho, inawezekana ukamheshimu mtu leo hata kama hastahili na kesho akawa msaada mkubwa tu kwako. Lakini tukijikweza leo, kesho tutaaibika. Usimuhemu huyu ukamuacha yule ukidhani unakuwa mwema zaidi. Heshimu wote ili uonekane mwenye heshima.

Onyesha heshima hata kwa watu wasiostahili; sio kwa muonekano wa tabia zao ila muonekano wa yako. Read Post »

Moyo wa Binadamu

By Maureen C. Minanago Je, unaufahamu kuwa kila mwanadamu anapumua kwa msaada wa moyo? Na je, unafahamu kuwa moyo huo huo unaweza kumfanya mtu kuwa na furaha ama huzuni? Hii ni alama ambayo wengi huitumia kuashiria moyo na moyo huo basi unatumika kama ishara ya upendo. Moyo ni pampu inayosukuma damu kupitia mishipa ya damu. Kupitia mishipa hiyo damu husambazwa mwili mzima ili kukupatia hewa safi (oxygen). Tukiachana na maswala ya kibaiolojia, moyo unakazi ya kupenda. Basi tuone upendo huo unaathiri vipi moyo na wewe kama binadamu unaukosea vipi moyo wako ama moyo wa mwingine. Jijali, mjali na mwenzio ili kuufurahisha moyo kwa afya zaidi. Huu ni moyo wa binadamu. Unapokuwa umezungukwa na watu wakupendao haijalishi ni upendo wa aina gani, moyo huwa na nguvu na hufanya kazi yake vizuri. Kila mmoja anapenda kupendwa, hata wababe huwa na wafuasi wao hata kama hawana upendo wa dhati. Moyo wenye furaha. Moyo wenye nguvu… Moyo wenye furaha huimba ndani yetu pale tunapoongeza marafiki wapya. Moyo wenye furaha huupoza mwili tusikiapo baridi yaani tuwapo wapweke, kwa kukumbuka mema mengi yaliyopita. Inawezekana kabisa kwa wewe kujichangamsha bila kusubiri kuchangamshwa. Moyo imara ni moyo wenye nguvu kwani unaweza kupigana na majaribu yote yanayotukumba katika maisha. Sisi sote tunapaswa kuwa na moyo wenye nguvu kwani pia ni rahisi kupingana na magonjwa tukianza na ugonjwa wa ‘moyo’ wenyewe. Upendo wa nguvu Upendo wa mahusiano ya kimapenzi ni upendo unaoleta hisia za kipekee. Kila mmoja anaweza kuuelezea ajuavyo yeye. LAKINI, maumivu ya kuachana kwa wapenzi hao yanaweza kuwa yanafanana kwani yote huumiza moyo. Upendo unaolega lega Afya ya mtu ni ya thamani, ni vema kutumia nafasi unayopata kwa mpenzi wako kumuonesha upendo na kupata upendo kutoka kwake. Kama unadhani hujaamua bado kujiingiza kwenye mahusiano, basi tafakari kabla ya kuchukua hatua. Ni vema kujiamini kwa ulifanyalo kuepukana na maumivu ya moyo. Kipindi tu unapojihusisha na mahusiano ya kimapenzi, fahamu kuwa unajifunga. Moyo uliofungwa kwa upendaye, usiufungulie kwa wengine. Angalizo: Ili kuulinda moyo (wako/mwemzako) na maumivu zingatia haya:- Ukipata mwenzako mshikilie sawa sawa. Ni bora kuumia kidole kitapona au kuvunjika kidole vingine vitafanya kazi lakini sio kuumia moyo sababu maumivu yake yaweza kuchukua miaka kuisha na kuvunjika kwa moyo ni ngumu kuutengeneza ukafanya kazi sawia. Kuna Moyo usioweza kufanya maamuzi sahihi, Moyo ulionyong’onyea na kudhoofika na Moyo uliochanganyikiwa. Hapa ndipo tunaposhauriwa kuwa na imani kwa kumuomba Mungu kwani yeye ndiye aliyekupa maisha. Jijali kwa kuepukana na athari hizo lakini pia, kama ikitokea ushaumizwa basi jitahidi kujishughulisha sana ili kupunguza mawazo. Kaa na watu watakupa mawazo tofauti usikae mwenyewe ukiwa mpweke kuepukana na mawazo potofu. Kemea roho ndani yako inayokusukuma kukata tamaa, kuchukia ama kujiua. Sali sana ukisikia hivyo kwa afya ya Roho na moyo pia. Maumivu makali ya moyo Usiuzeeshe moyo wako kwa mambo usiyoyaweza. Usiukondeshe kwa kuupa mambo mengi usiyoweza kuyafuatilia na kuyafanya kwa ufanisi, usiufanye ukaelemewa. Ujali moyo wako kwa kujipenda na kuwa makini. Lakini kikubwa, usiutegemee moyo pekee katika mapenzi, shirikisha akili yako. Ni kwa kufanya hivyo, moyo utabaki kupenda tu huku mengine yakifanywa kwa utashi uliobarikiwa nao.

Moyo wa Binadamu Read Post »

Urefu wa Kupindukia

By Maureen C. Minanago Wewe ni mrefu? Ni mara ngapi umekutana na watu warefu? Ni nini kinafanya mtu awe mrefu? Fuatilia….. Wanabiolojia wa molekuli (molecular biologists) wanaeleza kuwa tofauti ya urefu wa mtu na mtu kwa asilimia 60 mpaka 80 unatokana na maumbile huku asilimia 20 mpaka 40 unatokana na sababu za mazingira hasa lishe.  Urefu wa maumbile sana sana ni ule unaorithiwa hasa kutoka kwa mwanafamilia ama ndugu wa karibu. Kila mmoja anahomoni za ukuaji (somatotropin) ambazo zinamsababisha kurefuka haraka ama taratibu. Utofauti huu ndio unaoleta utofauti katika urefu wa mtu na mtu.Hizi homoni zina protini 191 zenye amino acid na uzito wa daltoni 22,124; na huzalishwa kwenye glandi iitwayo pituitary ambayo husambaza homini hizo mwilini kwa ajili ya ukuaji mara baada ya uzalishaji wake. Wengi wetu tutakumbuka msemo wa wazazi kwa watoto wao wa “lala ukue” kama kumuhamasisha aende kulala hasa wakati wa mchana ambapo watoto wengi hupenda kuutumia kucheza. Inawezekana baadhi wa wazazi wanautumia kama mazoea lakini msemo huo unaukweli ndani yake. Usambazaji wa homoni huchukua muda wa masaa matatu hadi matano lakini mtu hurefuka haraka ndani ya lisaa limoja tu akiwa amelala usingizi mzito. Hivyo ukuaji kutokea mara baada ya usambazaji wa homoni zinazohusika na ukuaji. Zikisambaa haraka na kwa wingi ndivyo mtu akuavyo mrefu zaidi kwa kipindi kifupi tu. Homoni hizi hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa watoto na vijana ambao wako katika kipindi cha ukuaji, na si kwa mtu mzima. Wazazi tuwashauri watoto wetu kupata usingizi wa kutosha ili kumsaidia kukua haraka. Yamkini hawa ni wapenzi, pamoja na kuwepo kwa tofauti zao kiurefu bado wanaonekana kupendana. (picha kushoto) Hawa nao ni marafiki, wao huchweza pamoja mpira wa kikapu. Wanaonekana kuwa wenye furaha sana ukiweka kando ukweli kuwa wamepishana sana urefu. (picha chini kulia) Hivyo, kama wewe ni mrefu kuzidi wenzako usijione wa tofauti sana, kaa nao, cheza nao, furahi pamoja nao na wala usijitenge kwani furaha yako ni furaha ya jamii nzima.Na kama wewe si mrefu usijishangae pia na wala usimtenge aliye mrefu zaidi yako. Kinachofanya mtu awe mkubwa zaidi au mdogo zaidi ni sehemu ya mbele ya glandi ya pituitary iitwayo ‘anterior pituitary’. Ikifanya kazi kupita kiwango humfanya mtu kuwa mrefu mno yaani ‘giant’ na vile vile inapofanya kazi chini ya kiwango basi mtu huwa mfupi zaidi yaani ‘dwarf’. Ewe kijana, unataka kuwa mrefu? Nawe mzazi, unataka mwanao arefuke vizuri? basi kama uko kwenye umri wa ukuaji bado unayo nafasi. Epukana na vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi (junk food). Pata lishe iliyobora kuisaidia glandi inayohusika na homoni za ukuaji kufanya kazi sahihi katika mwili wako. Hakikisha unapata usingizi wa kutosha ili kurahishisha somatotropin (homoni za ukuaji) kufanya mzunguko vizuri katika mfumo wake. Kunywa maziwa ili upate calcium itakayokuimarishia mifupa yako. Urefu ukiambatana na mifupa legevu unaweza kupata matege lakini ukipata calcium basi unakuwa imara muda wote. Kula vyakula vyenye amino acid mfano samaki, mayai, mboga mboga kama mabilinganya na matunda kama karoti matikiti na maepo.

Urefu wa Kupindukia Read Post »

Ufahamu Ugonjwa wa Kifua Kikuu – Tuberculosis (TB)

By Maureen C. Minanago JE, UNAUFAHAMU UGONJWA WA KIFUA KIKUU? Naibu meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma (2016), Dr. Liberate Mleoh, alielezea zaidi juu ya ugonjwa huu. Kifua kikuu (Tuberculosis-TB) kimegawanyika katika aina mbili; cha ndani ya mapafu na nje ya mapafu. Kifua kikuu cha ndani ya mapafu ndicho kinachojulikana zaidi na kinasumbua zaidi. Sasa je, kifua kikuu hiki kikoje? Ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea ambavyo vinamkuta mtu na kuharibu mapafu. Ugonjwa huu unaenea kwa njia ya hewa ambapo mtu mwenye vimelea hivyo anapokohoa ama kupiga chafya anaweza kumuambukiza mtu wa karibu naye ambaye hana vimelea hivyo.  Tanzania ni nchi ya ishirini na mbili inayoongoza kuwa na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu duniani lakini ni ya sita kwa Africa. Katika utafiti uliofanyika 2012 ili kujua ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu Tanzania, imegundulika kuwa, katika watu laki moja kuna wagonjwa wasiopungua 528 na uwezo wa watanzania kugundua wana kifua kikuu ni 36%. Ni jukumu la kila mmoja wetu basi kufuatilia kwa kupima mara kwa mara kama tatizo hilo lipo au la. Kama lipo basi matibabu yaanze mara moja ili kuepuka kuusambaza zaidi. Dr. Mleoh amesema mtu akitumia dawa kwa wiki mbili mpaka mwezi mmoja anapunguza hatari ya kumuambukiza asiye na vimelea vya ugonjwa. Sasa basi, kila mtu achukue hatua kwa afya yake. Kinachosababisha kifua kikuu ni mdudu (Mycobacterium Tuberculosis). Mdudu huyu anangozi ngumu kwa jina la utani wanasema “amevaa koti” hivyo inakuwa ngumu kumtibu kwa dawa ya kawaida. Dawa zinazotumika ni za mseto yaani ni zaidi ya moja. Mtaalamu anasema zinatumika dawa nne ndani ya kileo kimoja na inatumika kwa muda mrefu ambapo ni miezi sita mpaka nane kulingana na ukali wa tatizo; kama ni sugu basi dawa zitatumika kwa miezi isiyopungua ishirini. Ni zipi dalili za ugonjwa wa kifua kikuu? 1. Kukohoa mfururizo kwa wiki zisizopungua mbili; kikohozi cha kawaida ama kilichochanganyikana na damu.2.Kutokwa jasho lisilo la kawaida hasa kwa wakati wa usiku.3. Kukosa hamu ya kula.4. Kupungua uzito.5. Homa za jioni.6. Uchovu. Ugonjwa huu unatesa sana lakini unatibika. Pima afya yako sasa upate kujua kama uko salama au la. Kama uko salama basi jiepushe na uvutaji wa hewa kutoka kwa yeyote anayehohoa kwani huwezi jua yupi anavimelea vichanga. Lakini pia, kama wewe ni mmoja wa wagonjwa yaani umepima ukagundulika na vimelea vya tuberculosis mycobacterium basi jaribu kumkinga mwenzio kwa kuziba mdomo wakati unakohoa pamoja na kukohoa mbali naye. Tumia dawa ipasavyo  ili kuviua vimelea vyote mwilini kwa afya bora. Tatizo la watanzania wengi bado hawajaufahamu vizuri ugonjwa huu. Wewe uliyesoma mueleweshe na mwenzako. Kwa pamoja tutaweza kuutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu na kulinda miili yetu isidhoofike.  Kuwa Imara, jali afya yako.

Ufahamu Ugonjwa wa Kifua Kikuu – Tuberculosis (TB) Read Post »

Scroll to Top