UCHORAJI WA TATTOO

By Debora Mwangosi

Kuchora tattoo kuna maana tofauti kulingana na tamaduni na watu binafsi. Mara nyingi, ni njia ya kujieleza, kuonyesha maadili, au kumkumbuka mtu muhimu. Katika baadhi ya tamaduni, tattoo zinaweza kuwa alama za hadhi au ujasiri. Aidha, zinaweza pia kuwa na maana ya kiroho au kibinafsi, zikihusishwa na safari za maisha au matukio katika jamii.

Uchoraji wa tattoo hauna madhara tu, kwa upande mwingine tattoo zinafaida.

Kujieleza:

Tattoos hutoa nafasi ya kuonyesha mtindo wako wa maisha na thamani zako. Lakini jua kwamba kila mtu atakuwa na mtazamo juu ya tattoo yako siyo wote watakuwa na mtazamo ambao utakupendeza wengine watakuwa na mtazamo hasi.

Ukumbusho:

Zinatumika kukumbuka watu muhimu au matukio maalum katika maisha. Kila mtu ananjia yake ya kuweka kumbukumbu aidha kwa mtu, au tukio fulani. Lakini kwa kizazi hiki watu wengi sana hususani vijana wanapenda kutunza ukumbusho kwa kuchora tattoo ya tukio hilo.

Kujitambulisha:

Inaweza kuwa alama ya utambulisho wa kitamaduni au kikabila. Mfano mzuri tattoo aina ya kijamii [tribal tattoo] hizi hutambulisha mtu kuwa anatokea sehemu fulani kama vile ukiona mtu kajichora usoni alama za kiutamaduni basi moja kwa moja anaweza jua asili yake ni mmakonde hivyo hivyo kwa makabila mengine ambao wanatambulika kwa tattoo.

Kukuza sanaa:

Ni njia ya kuonyesha sanaa na ujuzi wa wabunifu wa tattoo lakini pia kukuza sanaa maana uchoraji wa tattoo ni moja ya sanaa na kuna watu wanajipatia kipato chao katika maisha kupitia uchoraji wa tattoo kwa watu.

Kwenye faida basi madhara hayakosekani. Hapa kuna baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kutokana na kuchora tattoo:

Maumivu:

Mchakato wa kuchora tattoo unaweza kuwa na maumivu, tofauti na mtu mmoja hadi mwingine. Na maumivu hutofautiana na aina ya tattoo ambayo unataka kuchora kuna aina zingine hazima maumivu makali ila kuna zingine maumivu yake ni makali kupelekea hata wengine kuishia njian.

Maambukizi:

Ikiwa vifaa havikutumika kwa usahihi au ikiwa tattoo haitatunzwa vizuri, kuna hatari ya maambukizi. Kama mchoraji atakuwa hana utazaji wa vifaa basi kuna uwezekano mkubwa sana wa watu kuambukizwa na magonjwa ambayo yana ambukizwa.

Mabadiliko ya Ngozi:

Tattoos zinaweza kuathiri ngozi kwa njia mbalimbali, kama vile kuwasha au kuvimba. Na hapa inategemea na kwa namna ngozi itaenda kupokea mabadiliko hayo kwa vifaa vinavyotumika ni vinatumia umeme, hivyo ngozi inakuwa hatarini kupata madhara yoyote.

Dhihirisho la Kijamii:

Katika baadhi ya jamii, tattoos zinaweza kuathiri nafasi za kazi au maoni ya watu wengine. Na asilimia ya kazi nyingi sana hawavutiwi na watu wenye tattoo kwasababu kwa namna moja ama nyingine  inaweza kuharibu picha ya taasisi. Lakini pia kwa upande wa jamii wazee wetu wanaamini uchoraji wa tattoo ni uhuni hivyo basi wanapomwona mtu kachora tattoo basi jamii inamtafsiri tofauti kidogo.           

“Vijana wanaelewa na kuthamini mabadiliko haya, na hivyo wanachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la tattoo. Sambamba na hayo vijana tuwe makini sana na mabadiliko ya utandawazi siyo kila kitu cha kuenda nacho maana kuna vitu utashindwa kufanya kwasababu ya makosa ambayo ulifanya kwasababu ya kuendana na utandawazi”.

Nini taswira ya jamii juu ya kuchora tattoo.

Taswira ya jamii juu ya kuchora tattoo inategemea sana tamaduni, mazingira ya kijamii, na historia ya eneo husika. Hapa kuna baadhi ya mitazamo tofauti:

  • Tamaduni za Kijadi:

Katika baadhi ya jamii, tattoo zinaweza kuzingatiwa kama ishara ya hadhi, ujira, au umuhimu wa kitamaduni. Ni sehemu ya mila na desturi.

  • Tabia za Kijamii:

Katika mazingira mengine, tattoo zinaweza kuonekana kama alama au uhuru wa kujieleza. Hapa, mtu anayechora tattoo anaweza kuonekana kama mwenye mtindo au jasiri. Hivyo basi mtu mwingine anakuwa huru akiwa na tattoo

  • Mipango ya Kijinsia:

Katika baadhi ya tamaduni, kuna mtazamo tofauti wa tattoo kati ya wanaume na wanawake. Kwa mfano, wanaume wanaweza kupewa uhalali zaidi katika kuchora tattoo kuliko wanawake wakiamini kuwa kwa mwanamke kuchora tattoo ni uhuni katika jamii.

  • Matarajio ya Kazi:

Katika mazingira ya kitaaluma, baadhi ya watu wanaweza kuangalia tattoo kwa jicho la hasi, wakiona kuwa zinaweza kuathiri nafasi za kazi au uhusiano wa kitaaluma. Kutokana na athari hii inapelekea watu wengine kuchora tattoo kwa kificho isiweze kuonekana mbele ya watu.

  • Ubunifu na Sanaa:

Wengine wanaona tattoo kama fomu ya sanaa na ubunifu, wakiheshimu uwezo wa wasanii wa tattoo na umuhimu wa kisanii katika maisha ya mtu. Na wengine wanaamini ni kazi kama kazi zingine katika jamii.

Msimamo wa jamii unaweza kubadilika kwa wakati, huku mabadiliko ya mtazamo wa kisasa yanaongeza kukubalika kwa tattoo katika jamii nyingi. Utandawazi unavyokuwa inapelekea kukuwa kwa kasi sana,

Kwa nini kundi la vijana linaongoza katika kuchora tattoo?

Athari za Utamaduni wa Kisasa:

Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vimeongeza umaarufu wa tattoo, na vijana wanaona wanavyoweza kuiga mitindo kutoka kwa wasanii maarufu. Ukuaji wa utandawazi unasababisha sana vijana kuiga vitu na kujaribu na kwa miaka inavyozidi kuendelea uchoraji wa tattoo utakuwa wa kawaida sana.

Jamii inayokuzunguka:

Vijana wengi huwa wanachora tattoo kutokana na jamii ambayo inamzunguka labda jamii anayoishi ina watu ambao wanapenda kuchora tattoo hii itamuhasisha kijana na yeye achore kwasababu ataona ni moja ya jamii hiyo.

Motisha kutoka kwa watu maarufu:

Watu maarufu wengi hususani waimbaji wa nyimbo wanafuatiliwa na vijana hivyo kutokana na mapenzi hayo hupelekea kijana kuiga kuona ni moja ya maisha kuchora tattoo labda pengine anaweza akavutia jamii kama wasanii wengine.

Kwa ujumla, vijana wanaelewa na kuthamini mabadiliko haya, na hivyo wanachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la tattoo. Sambamba na hayo vijana tuwe makini sana na mabadiliko ya utandawazi siyo kila kitu cha kuenda nacho maana kuna vitu utashindwa kufanya kwasababu ya makosa ambayo ulifanya kwasababu ya kuendana na utandawazi. Karne tunazoziendea ni lazima tuwe makini sana kwasababu vijanan watagemewa sana katika shughuli za kijamii lakini pia taifa kwa ujumla tukishwa kuchambua utandawazi ambao unabadilishwa kila siku taifa litakosa watu makini na uhodari wa kuongoza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top