Ufahamu Ugonjwa wa Kifua Kikuu – Tuberculosis (TB)

By Maureen C. Minanago JE, UNAUFAHAMU UGONJWA WA KIFUA KIKUU? Naibu meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma (2016), Dr. Liberate Mleoh, alielezea zaidi juu ya ugonjwa huu. Kifua kikuu (Tuberculosis-TB) kimegawanyika katika aina mbili; cha ndani ya mapafu na nje ya mapafu. Kifua kikuu cha ndani ya mapafu ndicho kinachojulikana zaidi na kinasumbua zaidi. Sasa je, kifua kikuu hiki kikoje? Ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea ambavyo vinamkuta mtu na kuharibu mapafu. Ugonjwa huu unaenea kwa njia ya hewa ambapo mtu mwenye vimelea hivyo anapokohoa ama kupiga chafya anaweza kumuambukiza mtu wa karibu naye ambaye hana vimelea hivyo.  Tanzania ni nchi ya ishirini na mbili inayoongoza kuwa na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu duniani lakini ni ya sita kwa Africa. Katika utafiti uliofanyika 2012 ili kujua ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu Tanzania, imegundulika kuwa, katika watu laki moja kuna wagonjwa wasiopungua 528 na uwezo wa watanzania kugundua wana kifua kikuu ni 36%. Ni jukumu la kila mmoja wetu basi kufuatilia kwa kupima mara kwa mara kama tatizo hilo lipo au la. Kama lipo basi matibabu yaanze mara moja ili kuepuka kuusambaza zaidi. Dr. Mleoh amesema mtu akitumia dawa kwa wiki mbili mpaka mwezi mmoja anapunguza hatari ya kumuambukiza asiye na vimelea vya ugonjwa. Sasa basi, kila mtu achukue hatua kwa afya yake. Kinachosababisha kifua kikuu ni mdudu (Mycobacterium Tuberculosis). Mdudu huyu anangozi ngumu kwa jina la utani wanasema “amevaa koti” hivyo inakuwa ngumu kumtibu kwa dawa ya kawaida. Dawa zinazotumika ni za mseto yaani ni zaidi ya moja. Mtaalamu anasema zinatumika dawa nne ndani ya kileo kimoja na inatumika kwa muda mrefu ambapo ni miezi sita mpaka nane kulingana na ukali wa tatizo; kama ni sugu basi dawa zitatumika kwa miezi isiyopungua ishirini. Ni zipi dalili za ugonjwa wa kifua kikuu? 1. Kukohoa mfururizo kwa wiki zisizopungua mbili; kikohozi cha kawaida ama kilichochanganyikana na damu.2.Kutokwa jasho lisilo la kawaida hasa kwa wakati wa usiku.3. Kukosa hamu ya kula.4. Kupungua uzito.5. Homa za jioni.6. Uchovu. Ugonjwa huu unatesa sana lakini unatibika. Pima afya yako sasa upate kujua kama uko salama au la. Kama uko salama basi jiepushe na uvutaji wa hewa kutoka kwa yeyote anayehohoa kwani huwezi jua yupi anavimelea vichanga. Lakini pia, kama wewe ni mmoja wa wagonjwa yaani umepima ukagundulika na vimelea vya tuberculosis mycobacterium basi jaribu kumkinga mwenzio kwa kuziba mdomo wakati unakohoa pamoja na kukohoa mbali naye. Tumia dawa ipasavyo  ili kuviua vimelea vyote mwilini kwa afya bora. Tatizo la watanzania wengi bado hawajaufahamu vizuri ugonjwa huu. Wewe uliyesoma mueleweshe na mwenzako. Kwa pamoja tutaweza kuutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu na kulinda miili yetu isidhoofike.  Kuwa Imara, jali afya yako.

Ufahamu Ugonjwa wa Kifua Kikuu – Tuberculosis (TB) Read Post »

Wewe ni wa Thamani

By Maureen C. Minanago Wewe ni wa Thamani!!! Jifunze umuhimu wako wewe kama binadamu kama utazingatia afya bora kwako na kwa mwenzako. Kula chakula chenye lishe na kufanya mazoezi ni changamoto kwa wengi hasa ukizingatia mfumo wa maisha kwa wengi hivi sasa. Lakini, ni afya njema tu itakayokupa nguvu ya kufanya yaliyo mazito na wepesi wa kufanya yaliyo magumu. Lishe inayoenda na mazoezi kiasi itakuepusha wewe na magonjwa kama kisukari, presha ya damu, unene wa kupindukia, kansa na mtindio wa ubongo. Badala yake hukupa vitu kama upeo mzuri wa kufikiri, nguvu, amani, wepesi, mzunguko mzuri wa damu na wa chakula, kwa kutaja machache. Mstari mmoja wa kitabu cha dini unasema “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”. Usijiachie ukasahau kutunza afya yako kwani wewe ni wa muhimu sana katika ulimwengu huu. Mungu hakukosea kukuumba hivyo ishi kwa kujali afya yako ili uwe na maisha yenye furaha. Magonjwa hututoa furaha, unene hutunyima uhuru kufanya baadhi ya vitu, kwa nini basi tusijitunze kwa kuzingatia lishe na mazoezi ili kupata afya na nguvu tele?! Usiwe nyuma katika kujua afya yako, pima mara kwa mara na ufanye tafiti hasa kwa kusoma nyaraka mbali mbali za afya ili uwe kwenye njia sahihi.

Wewe ni wa Thamani Read Post »

Fahamu Kuhusu Mayai

By Maureen C. Minanago Je, unafahamu kuwa yai hulainisha koo? Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapopikwa iwe kwa kukaangwa ama kwa kuchemshwa.Yai lina Vitamin D ambayo hupungua pindi lipikwapo. Hupungua kwa asilimia 90 likichemshwa sana hivyo kupoteza umuhimu wake kwa mwili wa binadamu. Sasa basi, ili kupata virutubisho vyote vya yai ni muhimu kulila likiwa bado bichi. Mayai mabichi ni mazuri kwa kula ili kupata lishe sahihi lakini kwa wale wenye aleji (allergy) mayai mabichi si sahihi kwao kwani inaongeza athari zaidi. Mayai pia huweza kuwa na vijidudu (bacteria) waitwao Salmonella enteritidis (SE) ambavyo vinatokana na ndege mwenyewe mfano kuku. Ni vizuri kuchunguza yai kabla ya kula ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza. Epuka kula mayai mabichi yaliyotagwa na kuku mgonjwa kwani ndio mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa na SE. Pata yai moja hadi mawili kwa siku. Yai halina shombo sana kwa hiyo ni rahisi kulinywa haraka likiwa bichi. Hizi ni faida za kula mayai kwa mwili wa binadamu:- Haishauriwi kutunza mayai katika friji ila yawekwe katika sehemu iliyopoa yaani ambayo haina joto kali wala baridi lililozidi. Ni muhimu kukagua yai kabla ya kulitumia hasa likiwa bichi; lakini sio tu kukagua mayai lakini kutumia mayai ya kienyeji kwani ndiyo yenye lishe zaidi. Usile yai:- Njia nzuri ya kupata yai salama ni kwa kufuga kuku mwenyewe na kama hutaweza kwa sababu mbalimbali basi nunua mayai kwa mtu anayefuga mwenyewe ili kuwa na uhakika wa usalama wa afya yako.

Fahamu Kuhusu Mayai Read Post »

Faida za Juisi ya Nyanya.

By Maureen C. Minanago Unafahamu umuhimu wa nyanya katika mwili wa binadamu? Nyanya ni tunda linaloliwa kwa njia mbali mbali. Wengine hutengenezea kachumbari, wengine huungia mboga, wengine hupikia rosti lakini wengine hupendelea kuisaga na kunywa juisi (juice). Tunda hili linafaida sana katika mwili wa binadamu. Lakini zaidi ni kama litatumika likiwa na virutubisho vyake vyote; yaani, likiwa bado bichi. Nyanya mbichi ni chanzo cha Vitamin A, Vitamin K, Vitamin B1, B2, B3, B5 na B6, pamoja na madini kama magneziam (magnesium), chuma (iron) na fosforas (phosphorus). Tafiti mbalimbali zimefanyika na kugundua kuwa, nyanya hasa katika mfumo wa maji ama kimiminika (liquor), inafaida. Moja kwa moja tuziangalie faida za juice ya nyanya kwa ngozi, nywele na afya ya mwili. Kabla ya kutengeneza tunda hili kwa chochote, hata kama litapikwa, hakikisha unaliosha kwa maji safi na salama kisha ulifute kwa kitambaa safi; ndipo ulitumie. Kitu cha kuzingatia ni usafi. Jaribu kutengeneza juice ya nyanya, jizoeshe kuinywa walau mara moja kwa wiki uone mabadiliko yenye mafanikio katika mwili wako.

Faida za Juisi ya Nyanya. Read Post »

Scroll to Top