“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”.

By Maureen C. Minanago Kuna ulemavu wa aina mbali mbali. Machache yajulikanayo ni kushindwa kutembea kushindwa kutumia mikono, kutoona vizuri ama kutoona kabisa, ulimi kuwa mzito hivyo kushindwa kuongea, kutosikia (kiziwi), mifupa kujikunja na kusababisha matege pamoja na kukosa melanin itengenezayo rangi ya ngozi (albino). Watu wenye ulemavu wanapaswa kujijali pia, wanapaswa kupata lishe iliyo bora kabisa ili kujikinga na maradhi. Hawapaswi kujihurumia na kujitenga, bali kuwa na jamii yao, hivyo kuwa na afya ya mwili na akili na kuwa na amani. Dkt. Abdallah Possi ni mtu mwenye albinism lakini anatumia fursa ya kuwa kiongozi kuielimisha jamii zaidi juu ya watu wenye ulemavu na kuwaasa waachane na mitazamo potofu ya kulionea kundi hilo.  Dkt Possi anasema, ”Kila mtu ni sawa lakini usawa huo uzingatie mtu na mtu; yaani, kila mtu aheshimiwe na kusikilizwa kulingana na nafasi ama hali aliyonayo”. Kundi la watu wenye walemavu limeonekana kuachwa nyuma kwani ni wachache na watu wengi wameonekana kuwaacha walio wachache na wale wachache wanajiona sio wa kawaida.  Amesema, ili kutibu historia ya muda mrefu ya watu wenye ulemavu kuachwa nyuma, haipaswi kuwepo kwa mtazamo wa upendeleo bali wachangamke ili kujitoa katika kundi walilomo kama; ilivyokuwa katika swala la wanawake.

“Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa”. Read Post »

AFYA ni nini?

By Maureen C. Minanago Afya ni hali ya kutokuwa na ugonjwa au kidonda. Afya ni hali ya kuwa na amani ya roho. Afya ni ubora wa akili, mwili na nafsi. Afya hutegemea vitu hivi vitatu ili kuwa hai na salama: Akili, Mwili, Nafsi. Akili ni utashi tuliopewa na Mwenyezi Mungu katika kung’amua mambo ulimwenguni. Akili hujumuisha uelewa, ufikiri, uamuzi na utendaji wa mambo. Hakuna awezaye kutafsiri akili yetu ila matendo yetu yanaweza kumfanya mtu aone flani yuko vipi; nayo bado itakuwa mtazamo wake sababu tunatofautiana kufikiri pia.  Binadamu hutumia akili kila siku na kila wakati ili kuelewa, kufikiri, kuamua na kuhakikisha tunatimiza jambo. Kwa maana hiyo, tunapaswa kuipumzisha “PUMZISHA AKILI”. Akili ikichoka mwili nao huchoka na hutafanya chochote sababu haitakuwa na uwezo mzuri kutenda. Lala au oga au ogelea au sikiliza mziki au chochote ukipendacho ambacho hakitakufanya utumie nguvu ya akili. Mwili ni muundo wote wa binaadam. Ni maumbile ya mtu. Mwili huhusisha yote yaliyotengeneza “mtu” mfano viungo kama miguu, mikono n.k, Maji kama mate, damu n.k, na vingine kama mishipa kucha na nywele. Tunapaswa kujipenda kwa kula vizuri, kulala vizuri na pazuri, kuvaa vizuri na kujijali muda wote kwa kuuweka mwili salama mfano kwa kupiga mswaki baada ya kula, kuosha nywele mara kwa mara, kukata na kusafisha kucha, kuoga, na kuvaa nguo safi. Pia tujiepushe na hatari, ugomvi na makwazo kwa faida ya mioyo yetu.  Ukitembea sana juani pata kivuli unywe na maji. Penye baridi uvike mwili wako kwa sweta ama nguo nzito. Ukiumia au kuumwa pata matibabu sahihi kwa kwenda hospitalini. Jipende, Ujali mwili wako. Tukifanya hivyo miili yetu itakuwa salama.  Nafsi ni roho yenye kuleta imani ndani yetu. Sisi huamini vitu mbali mbali kwa msaada wa nafsi. Lakini yote heri kama tutaamini vitu vyenye kujenga na sio kubomoa. Nafsi pia hutofautiana ya mtu na mwingine ndio maana tukawa tofauti japo chimbuko letu kiuumbaji ni moja.  Nafsi nayo huhitaji utulivu ili kuupa mwili na akili nguvu za kuishi kwa afya. Pata muda wa kutulia ukiongea na WEWE kujua nini waweza fanya LAKINI, mshirikishe MUUMBA wako kwa yote kupata amani uitakayo moyoni na kwa wakuzungukao. Hivyo basi, jipe likizo au omba likizo. Tembelea sehemu mbali mbali za starehe au vivutio kutuliza mwili, akili na roho pia. Ongea vizuri na watu, cheka, tabasamu hata kama umeumizwa. Inasaidia sana.  Afya ya vitu vyote vitatu ni muhimu katika kukuweka mwenye nguvu na furaha.  Jali afya yako!

AFYA ni nini? Read Post »

Onyesha heshima hata kwa watu wasiostahili; sio kwa muonekano wa tabia zao ila muonekano wa yako.

By Maureen C. Minanago Maneno ya Dave Willis yanakumbushia utoaji wa heshima. Waswahili wanasema “heshima ni kitu cha bure” yaani huhitaji kulipia wala kugharamia chochote kuheshimu ama kuheshimiwa ila kujiheshimu na kutoa heshima hiyo kwa wengine wote hata kama hawastahili heshima yako. Inakuwaje mtu hastahili heshima yako? Ni kwa sababu haonyeshi upendo kwako kama binadamu, sababu anakuona uko chini sana, sababu anakudharau, anakuona hufai kwake na katika maisha yake, sababu huna uwezo kifedha ama kifikra, sababu huwezi kufika alipofika, sababu hujampa alichotaka, hauna muonekano mzuri na mengine mengi. Zipo sababu nyingi lakini pamoja na yote tunapaswa kukumbuka kuwa sote ni binadamu na tunakosea. Inawezekana tukapishana leo  lakini tukumbuke dunia huzunguka, binadamu pia. Tuheshimiane kwani hatujui ya kesho, inawezekana ukamheshimu mtu leo hata kama hastahili na kesho akawa msaada mkubwa tu kwako. Lakini tukijikweza leo, kesho tutaaibika. Usimuhemu huyu ukamuacha yule ukidhani unakuwa mwema zaidi. Heshimu wote ili uonekane mwenye heshima.

Onyesha heshima hata kwa watu wasiostahili; sio kwa muonekano wa tabia zao ila muonekano wa yako. Read Post »

2024 Health Care Excellence Symposium

Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) – Ruaha Hall, Dar Es Salaam, Tanzania. Start: Monday, 15 Jul, 2024 @ 8:00 am End: Tuesday, 16 Jul, 2024 @ 5:00 pm Organizer Information AHEAD, Inc Adventures in Health, Education, and Agricultural Development is a 501(c)(3) qualified non-profit and non-governmental organization based in Rockville, Maryland with affiliates in Tanzania, The Gambia and Bermuda. Contact Information  Phone: +255754099127  Email: ngozimatrona@gmail.com Ticket Information | READ MORE HERE

2024 Health Care Excellence Symposium Read Post »

Kazana

By Maureen C. Minanago Endelea kukimbia hata kama ni wa mwisho katika mashindano. Huwezi jua, yawezekama ukawa bingwa. Ninawakummbusha ndugu zanguni kutokata tamaa maana muda unaokata tamaa unaweza kuwa ndio muda sahihi kabisa kwa wewe kupata mafanikio/ ukitakacho/ ulichoomba kwa muda mrefu/ kufikia ndoto zako na kadhalika. Ukihisi kuacha usiache, kazana kwa kuwa umekaribia. Sote ni washindi kwa muda tofauti na kwa namna tofauti.

Kazana Read Post »

KUMBATO NI TIBA

By Maureen C. Minanago Kumbato mara nyingi hutumika tunaposalimiana ama kuagana kwa furaha na wapendwa wetu. Hii ni ishara ya furaha na mara nyingi huchukua sekunde chache sana kama 3 mpaka 6.  Tunaposalimiana kwa mikono tunakuwa na umbali kiasi flani na ndiyo maana tunapokuwa makazini ama tukikutana na watu kwa mara ya kwanza tunapeana mikono kwa kuwa hatujawa karibu kiasi cha kuonyesha hisia zetu hasa za furaha kwao. Kitendo cha kukumbatia ni sehemu mojawapo ya kudumisha upendo kati yetu na tuwapendao. Na kumbato hilo hilo hugeuka kuwa tiba hasa tunapotumia sekunde nyingi zaidi walau 20 na kuendelea. Unapomkumbatia mtu ipasavyo, unakuwa na nafasi kubwa sana ya kuondoa ugonjwa, kutuliza hasira, kutuliza au kuondoa shauku, kutoa upweke, kupoteza huzuni na hata kupunguza na kuondoa kabisa msongo wa mawazo. Tuangalie manufaa ya kumbato kwa undani wake: Malezi yanayohusisha mguso wa kumbato hujenga hali ya uaminifu na hisia ya usalama. Hii husaidia kuleta mawasiliano ya wazi na yenye uaminifu. Kumbato linaweza kuongeza kiwango cha Oxytocin papo hapo na kukuinulia hisia chanya. Nayo hutoa hisia ya upweke, kutengwa, shauku kali na hasira. Kukumbatia kwa muda mrefu hunyanyua viwango vya Serotonin hivyo kuinua mudi ya kujenga furaha. Kumbato huimarisha mfumo wa kinga hivyo kukulinda na magonjwa. Shinikizo la taratibu katika Sternum na chaji za hisia, hujenga na kufanya Solar Plexus Chakra kuwa hai hivyo kuchochea kongosho tezi, ambayo husimamia uzalishwaji wa seli nyeupe za damu mwilini. Solar Plexus Chakra ni msingi wa utu wetu, utambulisho wetu na u-sisi wetu.  Unapokumbatia unalegeza mishipa. Hii huondoa mvutano mwilini mwako na kukuondolea maumivu kwa kuongeza mzunguko katika tishu laini hivyo kukupoza na kukupa tulizo. Kumbato huweka usawa katika mfumo wa neva. Majibu ya mtu ya ngozi ya Galvanic katika kutoa na kupokea kumbato huonyesha mabadiliko ya nguvu katika ngozi. Athari ndani ya unyevu na umeme katika ngozi hupendekeza hali ya usawa zaidi katika mfumo wa neva. Ni jambo linalotufundisha kutoa na kupokea. Ukikumbatiana na mtu au watu unapata thamani ya usawa ya kutoa na kupokea joto kama kutoa na kugawana. Inaelimisha juu ya upendo kwa wote wakumbatianao (wawili, watatu au kundi). Kukumbatiana ni kama tafakari ya undani au kicheko cha furaha ambavyo kufdunza kusahau ama kupotezea yale yanayobugudhi, yanayokwaza au kuumiza na kujikita katika usasa yaani kuishi kwa wakati uliopo.  Kumbato hukufanya ujisikie uko hai. Hukupa mzunguko wa mawazo mbalimbali yaliyo katika maumbo tofauti na kukuunganisha na moyo pamoja na pumzi yako. Kumbato huletea hali ya kujiamini. Hali ambayo imekaa ndani yetu toka udogo wetu ambapo tumekuwa tukikumbatiwa na kubebwa kwa upendo na wapendwa wetu kama ndugu jamaa na marafiki. Hisia hizi zimekuwa ndani yetu kadiri tukuavyo hivyo kutujengea nguvu na uwezo wa kujipenda. Kumbato la nguvu linalogusisha mioyo ya wawili wakumbatianao hufanya upendo kati yao kuwa maradufu hivyo kuweka uzio usioweza kuwatenganisha kirahisi kwani upendo ni dawa ya ajabu.  Kumbato pia huimarisha saikolojia yetu na kuleta maendeleo ya miili yetu kwani hukufanya tulivu na mwenye afya ya roho na mwili pia. Nguvu unayobadilishana na umkumbatiaye huwekezwa katika mahusiano yenu (mama na mwana, baba na mwana, marafiki, kaka na dada, wapenzi na kadhalika). Nguvu hiyo huleta hamasa ya uelewa baina yenu na mwisho kuwafanya mdumu. Pia husaidia kunyoosha misuli ya nyuso, kuondoa mikunjo ya uzee pamoja na kufanya uzee uje taratibu ama kupunguza kasi ya uzee. Varginia Satir ni mtaalamu anayeheshimika katika mambo ya familia. Yeye aliweza kufanya utafiti mdogo na kujiwekea msemo ambao sote tukiuzingatia tunaweza imarisha afya zetu kwa kiwango fulani. Anasema: *Tunahitaji kumbato mara 4 kwa siku ili KUISHI * Tunahitaji kumbato mara 8 ili KUREKEBISHIKA / KUIMARIKA *Tunahitaji kumbato mara 12 ili KUKUA Kwa wale wapendanao (wapenzi), kumbato ni chanzo kikubwa cha kuboresha mahusiano yenu  na tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, wapenzi wanaokumbatiana sana hudumu kwenye mahusiano yao kwa muda mrefu. Tibu maumivu yako sasa, tibu upweke na hali zote mbaya unazozipata kwa kupata kumbato. Anza kukumbatia watu zaidi kwa tiba rahisi zaidi.

KUMBATO NI TIBA Read Post »

Moyo wa Binadamu

By Maureen C. Minanago Je, unaufahamu kuwa kila mwanadamu anapumua kwa msaada wa moyo? Na je, unafahamu kuwa moyo huo huo unaweza kumfanya mtu kuwa na furaha ama huzuni? Hii ni alama ambayo wengi huitumia kuashiria moyo na moyo huo basi unatumika kama ishara ya upendo. Moyo ni pampu inayosukuma damu kupitia mishipa ya damu. Kupitia mishipa hiyo damu husambazwa mwili mzima ili kukupatia hewa safi (oxygen). Tukiachana na maswala ya kibaiolojia, moyo unakazi ya kupenda. Basi tuone upendo huo unaathiri vipi moyo na wewe kama binadamu unaukosea vipi moyo wako ama moyo wa mwingine. Jijali, mjali na mwenzio ili kuufurahisha moyo kwa afya zaidi. Huu ni moyo wa binadamu. Unapokuwa umezungukwa na watu wakupendao haijalishi ni upendo wa aina gani, moyo huwa na nguvu na hufanya kazi yake vizuri. Kila mmoja anapenda kupendwa, hata wababe huwa na wafuasi wao hata kama hawana upendo wa dhati. Moyo wenye furaha. Moyo wenye nguvu… Moyo wenye furaha huimba ndani yetu pale tunapoongeza marafiki wapya. Moyo wenye furaha huupoza mwili tusikiapo baridi yaani tuwapo wapweke, kwa kukumbuka mema mengi yaliyopita. Inawezekana kabisa kwa wewe kujichangamsha bila kusubiri kuchangamshwa. Moyo imara ni moyo wenye nguvu kwani unaweza kupigana na majaribu yote yanayotukumba katika maisha. Sisi sote tunapaswa kuwa na moyo wenye nguvu kwani pia ni rahisi kupingana na magonjwa tukianza na ugonjwa wa ‘moyo’ wenyewe. Upendo wa nguvu Upendo wa mahusiano ya kimapenzi ni upendo unaoleta hisia za kipekee. Kila mmoja anaweza kuuelezea ajuavyo yeye. LAKINI, maumivu ya kuachana kwa wapenzi hao yanaweza kuwa yanafanana kwani yote huumiza moyo. Upendo unaolega lega Afya ya mtu ni ya thamani, ni vema kutumia nafasi unayopata kwa mpenzi wako kumuonesha upendo na kupata upendo kutoka kwake. Kama unadhani hujaamua bado kujiingiza kwenye mahusiano, basi tafakari kabla ya kuchukua hatua. Ni vema kujiamini kwa ulifanyalo kuepukana na maumivu ya moyo. Kipindi tu unapojihusisha na mahusiano ya kimapenzi, fahamu kuwa unajifunga. Moyo uliofungwa kwa upendaye, usiufungulie kwa wengine. Angalizo: Ili kuulinda moyo (wako/mwemzako) na maumivu zingatia haya:- Ukipata mwenzako mshikilie sawa sawa. Ni bora kuumia kidole kitapona au kuvunjika kidole vingine vitafanya kazi lakini sio kuumia moyo sababu maumivu yake yaweza kuchukua miaka kuisha na kuvunjika kwa moyo ni ngumu kuutengeneza ukafanya kazi sawia. Kuna Moyo usioweza kufanya maamuzi sahihi, Moyo ulionyong’onyea na kudhoofika na Moyo uliochanganyikiwa. Hapa ndipo tunaposhauriwa kuwa na imani kwa kumuomba Mungu kwani yeye ndiye aliyekupa maisha. Jijali kwa kuepukana na athari hizo lakini pia, kama ikitokea ushaumizwa basi jitahidi kujishughulisha sana ili kupunguza mawazo. Kaa na watu watakupa mawazo tofauti usikae mwenyewe ukiwa mpweke kuepukana na mawazo potofu. Kemea roho ndani yako inayokusukuma kukata tamaa, kuchukia ama kujiua. Sali sana ukisikia hivyo kwa afya ya Roho na moyo pia. Maumivu makali ya moyo Usiuzeeshe moyo wako kwa mambo usiyoyaweza. Usiukondeshe kwa kuupa mambo mengi usiyoweza kuyafuatilia na kuyafanya kwa ufanisi, usiufanye ukaelemewa. Ujali moyo wako kwa kujipenda na kuwa makini. Lakini kikubwa, usiutegemee moyo pekee katika mapenzi, shirikisha akili yako. Ni kwa kufanya hivyo, moyo utabaki kupenda tu huku mengine yakifanywa kwa utashi uliobarikiwa nao.

Moyo wa Binadamu Read Post »

Urefu wa Kupindukia

By Maureen C. Minanago Wewe ni mrefu? Ni mara ngapi umekutana na watu warefu? Ni nini kinafanya mtu awe mrefu? Fuatilia….. Wanabiolojia wa molekuli (molecular biologists) wanaeleza kuwa tofauti ya urefu wa mtu na mtu kwa asilimia 60 mpaka 80 unatokana na maumbile huku asilimia 20 mpaka 40 unatokana na sababu za mazingira hasa lishe.  Urefu wa maumbile sana sana ni ule unaorithiwa hasa kutoka kwa mwanafamilia ama ndugu wa karibu. Kila mmoja anahomoni za ukuaji (somatotropin) ambazo zinamsababisha kurefuka haraka ama taratibu. Utofauti huu ndio unaoleta utofauti katika urefu wa mtu na mtu.Hizi homoni zina protini 191 zenye amino acid na uzito wa daltoni 22,124; na huzalishwa kwenye glandi iitwayo pituitary ambayo husambaza homini hizo mwilini kwa ajili ya ukuaji mara baada ya uzalishaji wake. Wengi wetu tutakumbuka msemo wa wazazi kwa watoto wao wa “lala ukue” kama kumuhamasisha aende kulala hasa wakati wa mchana ambapo watoto wengi hupenda kuutumia kucheza. Inawezekana baadhi wa wazazi wanautumia kama mazoea lakini msemo huo unaukweli ndani yake. Usambazaji wa homoni huchukua muda wa masaa matatu hadi matano lakini mtu hurefuka haraka ndani ya lisaa limoja tu akiwa amelala usingizi mzito. Hivyo ukuaji kutokea mara baada ya usambazaji wa homoni zinazohusika na ukuaji. Zikisambaa haraka na kwa wingi ndivyo mtu akuavyo mrefu zaidi kwa kipindi kifupi tu. Homoni hizi hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa watoto na vijana ambao wako katika kipindi cha ukuaji, na si kwa mtu mzima. Wazazi tuwashauri watoto wetu kupata usingizi wa kutosha ili kumsaidia kukua haraka. Yamkini hawa ni wapenzi, pamoja na kuwepo kwa tofauti zao kiurefu bado wanaonekana kupendana. (picha kushoto) Hawa nao ni marafiki, wao huchweza pamoja mpira wa kikapu. Wanaonekana kuwa wenye furaha sana ukiweka kando ukweli kuwa wamepishana sana urefu. (picha chini kulia) Hivyo, kama wewe ni mrefu kuzidi wenzako usijione wa tofauti sana, kaa nao, cheza nao, furahi pamoja nao na wala usijitenge kwani furaha yako ni furaha ya jamii nzima.Na kama wewe si mrefu usijishangae pia na wala usimtenge aliye mrefu zaidi yako. Kinachofanya mtu awe mkubwa zaidi au mdogo zaidi ni sehemu ya mbele ya glandi ya pituitary iitwayo ‘anterior pituitary’. Ikifanya kazi kupita kiwango humfanya mtu kuwa mrefu mno yaani ‘giant’ na vile vile inapofanya kazi chini ya kiwango basi mtu huwa mfupi zaidi yaani ‘dwarf’. Ewe kijana, unataka kuwa mrefu? Nawe mzazi, unataka mwanao arefuke vizuri? basi kama uko kwenye umri wa ukuaji bado unayo nafasi. Epukana na vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi (junk food). Pata lishe iliyobora kuisaidia glandi inayohusika na homoni za ukuaji kufanya kazi sahihi katika mwili wako. Hakikisha unapata usingizi wa kutosha ili kurahishisha somatotropin (homoni za ukuaji) kufanya mzunguko vizuri katika mfumo wake. Kunywa maziwa ili upate calcium itakayokuimarishia mifupa yako. Urefu ukiambatana na mifupa legevu unaweza kupata matege lakini ukipata calcium basi unakuwa imara muda wote. Kula vyakula vyenye amino acid mfano samaki, mayai, mboga mboga kama mabilinganya na matunda kama karoti matikiti na maepo.

Urefu wa Kupindukia Read Post »

Fahamu Faida za Maziwa Mtindi

By Maureen C. Minanago Maziwa mtindi yanavirutubisho vingi sana vinavyopendkezwa kuwa na faida nyingi katika mwili wa binadamu. Ni lini mara yako ya mwisho kupata maziwa mtindi? Pata kama chakula ama baada ya chakula ama kabla ya chakula, yatakusaidia. Soma faida zake hapa. Kabla ya kuzifahamu faida ya maziwa mtindi kwanza tuone virutubisho vichache vinavyopatikana ndani yake. Mtindi una calcium, phosphous, riboflavin (vitamin B2), iodine, vitamin B12. panantothenic acid (vitamin B5) zinc, potassium pamoja na molybdenum. Mbali na virutubisho hivyo, maziwa mtindi pia yana wadudu ambao ni “bakteria hai” wenye umuhimu mwilini kiafya.  Kuna homoni (cortisol) sehemu ya katikati ya tumbo na kiuno ambayo inakazi ya kuamuru ubongo kuongeza mafuta chini ya tumbo hivyo kusababisha kitambi.  Maziwa mtindi husaidia kupunguza ama kuondoa kabisa kitambi Kwa asilimia 82; kwa msaada wa madini ya calcium yaliko kwenye mtindi ambayo hupunguza homoni inayoamuru mafuta kwenda chini ya kiuno. Ni vema kunywa kutumia maziwa mtindi mara moja moja hasa wakati wa jioni unapokuwa umepumzika yaani baada ya shughuli zako. Pata mtindi ukiambatanisha na maji mengi ili kurahisisha mfumo wa upatikanaji wa maji mwilini. Mtindi huufanya mwili kuwa na maji muda wote yaani usiwe mkavu. Faida zingine ni pamoja na:  Kurefusha Maisha Kwani yanauwezo wa kupambana na magonjwa.Ni kinga kwa kina mama kwani inakinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections).Ni kinga ya mwili kwani inapambana na magonjwa kama saratani mfano saratani ya utumbo.Kuondoa lehemu (cholesterol) mbaya mwilini hilo kumuepusha mtu na tatizo la shinikizo la damu.Kupunguza uzito kwa asilimia 22 kwani yanapunguza mafuta mwilini.Yanasaidia kukupa seli za misuli yako kupitia virutubisho vya protini.Yanasaidia kuupa mwili nguvu kupitia virutubisho vya wanga.Chonde: Usitumie maziwa ya mtindi yatokanayo  na maziwa ya unga kwani utakosa ule uchachu na bakteria hai wenye umuhimu mwilini, hivyo kukosa virutubisho mwilini.  Unaweza pata maziwa mtindi kama mboga ukala na ugali, unaweza kuyanywa yenyewe kama chakula, unaweza kuyanywa na kitafunwa kama biskuti, mkate au maandazi. Wengi wetu hupenda kupunguza miili kwa mazoezi lakini jambo kubwa tunalosahau ni lishe bora na / mlo kamili. Ukifanya mazoezi ukaendelea kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi, hutakuwa umepunguza tatizo. Fanya mazoezi kisha pata maziwa mtindi ujionee tofauti. 

Fahamu Faida za Maziwa Mtindi Read Post »

Scroll to Top