Kasa mbstrinitycare

Kasa: Mnyama mpole mwenye maajabu mengi

By Nasibu Mahinya Karibu kila mnyama wa ardhini ana ndugu yake wa majini ambaye hufanana naye kimuonekano na hata tabia wakati mwingine. Ukiona kobe anaogelea basi jua mapema kuwa huyo siyo kobe, huyo ni kasa. Kasa ni mnyama wa majini ambaye wengi humfananisha na kobe kwa sababu ya ufanano wao wa zaidi ya asilimia 90. Kasa ni mnyama mkongwe ambaye anasemekana kuwepo duniani kwa zaidi ya miaka millioni mia. Wengi wamekuwa wakimuita ‘kobe wa majini’ au ‘kobe maji’ na inajulikana hivyo lakini hawa ni wanyama wawili tofauti na leo nitakupa sifa tisa za kasa ili tuweze kumjua zaidi kiumbe huyu. 1. Kasa ni mnyama wa majini ambaye hutaga mayai yake ardhini na ana tabia ya kuyafukia mayai yake kwa mchanga ufukweni. 2. Kasa hujamiiana kipindi cha miezi ya Machi mpaka Oktoba yani mwezi wa tatu hadi wa kumi. 3. Kasa huja nchi kavu kutaga mayai na kuyafukia tu na kisha kuondoka bila kurudi tena. Hutaga zaidi ya mayai sabini ambayo hutotoa ndani ya siku sitini. 4. Mayai ya kasa hutotoa yakiwa yamefukiwa na mchanga hivyo kumlazimisha kinda wa kasa kufukua na kuibuka kutoka mchangani na kuanza kuelekea majini. 5. Jinsia ya kasa anayetotolewa hutegemea na joto la mchanga. Zikizidi nyuzi joto 30° basi yai hutotoa jike na zinapopungua nyuzi joto 30° basi yai hutotoa dume. Uzao wa makasa jike umekuwa ukiathiriwa katika maeneo  yanayokumbwa na majanga ya tabianchi, hivyo kusababisha ongezeko la joto na matokeo yake ni upungufu wa makasa jike na kuathiri uzao wao kwa ujumla.  6. Mara nyingi kasa jike hurudi kutaga mayai pale alipototolewa yeye. Kama kabila flani wanavyorudi kwao kila ifikapo Krismasi hahahah! Natania. 7. Idadi kamili ya kasa waliopo duniani haijulikani kwa sababu kasa dume huwa hawarudi tena nchi kavu baada ya kutotolewa hivyo ni ngumu kuwahesabu. 8. Kasa anaweza kuwa na uzito wa hadi kilo 900 na anaweza kuishi mpaka miaka 80. 9. Tofauti na alivyo kobe, kasa hawezi kuingia ndani ya jumba lake, hivyo kichwa na miguu yake hubaki nje ya gamba muda wote. Kasa wanapatikana kwa wingi visiwani Zanzibar na Mafia. Unaweza kucheza nao na kuogelea nao kwenye bwawa maalum au baharini chini ya maji. 

Kasa: Mnyama mpole mwenye maajabu mengi Read Post »

JINSI MITANDAO YA KIJAMII INAVYOWEZA KUATHIRI AFYA YA AKILI mbstrinitrycare

JINSI MITANDAO YA KIJAMII INAVYOWEZA KUATHIRI AFYA YA AKILI

By Slyvia Mtenga Mitandao ya kijamii imeleta mapinduzi makubwa katika mawasiliano, mahusiano, na maisha ya kila siku kwa watu wengi ulimwenguni. Ingawa imeleta manufaa makubwa kama kuunganisha watu, kushiriki habari kwa urahisi, na kutoa majukwaa ya kujifunza na kujiburudisha, pia imezua changamoto zinazohusiana na afya ya akili. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa kutumia mitandao ya kijamii kwa muda mrefu na kwa njia zisizo sahihi kunaweza kuathiri afya ya akili ya watumiaji kwa njia tofauti. Hapa tunachambua jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuathiri afya ya akili kwa undani zaidi. 1. Shinikizo la Kulinganisha Maisha Mitandao ya kijamii imejaa picha, video, na machapisho ambayo mara nyingi huonyesha maisha ya kupendeza na yenye mafanikio. Watumiaji wengi hujilinganisha na wenzao ambao huonekana kuishi maisha mazuri, hali inayoweza kuathiri hisia za kujithamini kwa wanaotazama. Kwa watu ambao wanakabiliana na changamoto za maisha, kulinganisha huku kunaweza kusababisha hisia za kutoridhika na maisha yao wenyewe, kushuka moyo, na hata huzuni kali. 2. Kuathiri Usingizi Kutumia mitandao ya kijamii kabla ya kulala kunaweza kuathiri ubora wa usingizi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa mwanga unaotokana na skrini za simu na kompyuta unachangia kupunguza usiri wa homoni ya usingizi (melatonin), na hivyo kusababisha watu kuwa na changamoto za kulala vizuri. Ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha uchovu wa akili, na kuchangia matatizo mengine kama wasiwasi, huzuni, na hisia za kutopenda kazi au shughuli za kawaida. 3. Kutengwa na Jamii Ingawa mitandao ya kijamii inalenga kuunganisha watu, mara nyingi inaweza kupelekea kutengwa kwa kijamii. Watumiaji wanaweza kujikuta wanatumia muda mwingi mtandaoni badala ya kuwa na mwingiliano wa ana kwa ana na marafiki na familia. Hali hii inaweza kuchangia upweke, hali ambayo ni hatari kwa afya ya akili na inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiakili kama huzuni na wasiwasi. 4. Kushuka Kwa Hisia za Kujiamini Unyanyasaji wa mtandaoni (cyberbullying) ni tatizo lingine kubwa linalochangiwa na mitandao ya kijamii. Maneno na ujumbe mbaya, kejeli, na maoni yasiyofaa yanaweza kumfanya mtu kuwa na hisia za kutojiamini na kutokuwa na thamani. Haswa kwa vijana ambao bado wanaendelea kujenga utu wao, unyanyasaji huu unaweza kusababisha athari kubwa kwa afya ya akili, ikiwemo matatizo ya huzuni na hata mawazo ya kujiua. 5. Shinikizo la Kuwa Mkamilifu Katika mitandao ya kijamii, watumiaji wengi hujaribu kuonyesha sura nzuri zaidi ya maisha yao, hali ambayo inaweza kusababisha shinikizo kwa wengine kuwa na maisha “kamili.” Watu wanaweza kuhisi wanalazimika kujiwasilisha kwa njia fulani ili kukubalika na kuwa na wafuasi wengi. Shinikizo hili linaweza kusababisha wasiwasi, kujidharau, na kutokujikubali. 6. Kuathiri Afya ya Akili kwa Vijana Vijana na vijana wadogo wanaonekana kuwa kundi lililo hatarini zaidi kutokana na kutumia mitandao ya kijamii kupita kiasi. Kwa kuwa wako katika hatua ya kujenga utambulisho wao, wanaweza kuwa rahisi kuathiriwa na maoni ya wengine kuhusu wao. Kujisikia kutengwa au kutothaminiwa katika mitandao ya kijamii kunaweza kuathiri sana ukuaji wao wa kiakili na kihisia. Njia za Kuepuka Athari za Mitandao ya Kijamii kwa Afya ya Akili Kwa ujumla, mitandao ya kijamii ni zana yenye nguvu inayoweza kuleta athari chanya na hasi kwa afya ya akili. Ni muhimu kutumia mitandao hii kwa busara na kwa kuweka mipaka ili kuweza kunufaika nayo bila kudhuru afya ya akili. Kadri teknolojia inavyoendelea kuingia katika maisha yetu, ni muhimu kuwa na uelewa wa athari zake na kujifunza mbinu za kudhibiti matumizi yake ili kulinda afya ya akili.

JINSI MITANDAO YA KIJAMII INAVYOWEZA KUATHIRI AFYA YA AKILI Read Post »

Changamoto baada ya kumaliza chuo mbstrinitycare

CHANGAMOTO ZA VIJANA WANAOTOKA CHUO NA KUKABILIANA NA MAISHA MTAANI.

By JAMES MANJECHE Vija wanaomaliza masomo yao vyuoni mara nyingi hukutana na hali halisi, tofauti kabisa na matarajio waliyokuwa nayo wakiwa masomoni. Wengi huingia mtaani wakiwa na ndoto kubwa za kufanikisha maisha, lakini changamoto nyingi huwazuia kufikia malengo yao kwa haraka.  Mimi kama shuhuda mmoja wapo, vijana wengi tunakumbana na chanagmoto nyingi baada tu ya kutoka vyuoni. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto;   UKOSEFU WA AJIRA Moja ya changamoto kubwa inayowakumba vijana ni ukosefu wa ajira. Wanafunzi wengi huamini kuwa kupata shahada ni tiketi ya moja kwa moja ya kupata kazi nzuri, lakini hali halisi ni tofauti. Uchumi wa nchi nyingi, hasa barani Afrika ikiwemo Tanzania, hauwezi kutoa nafasi za kazi za kutosha kwa wahitimu wote.   UKOSEFU WA UJUZI WA KAZI  Licha ya kuwa na elimu ya darasani, wahitimu wengi wanakosa ujuzi wa vitendo unaohitajika katika soko la ajira. Waajiri wengi huweka kipaumbele kwa watu wenye uzoefu wa kazi, jambo linalowaweka wahitimu katika hali ngumu ya kuanza kazi.  Kwa mfano: Waanafunzi wengi wanaomaliza shahada ya biashara katika vyuo vya biashara wanajikuta wakishindwa katika mahojiano ya kazi (Interview) kwa sababu yakutokuwa na uzoefu wa kutosha wa kutumia programu za kifedha ambazo waajiri walihitaji.   KUKOSEKANA KWA MITAJI YA KUANZISHA BIASHARA  Kwa baadhi ya vijana, changamoto ya ajira huwafanya kufikiria kuanzisha biashara zao wenyewe. Hata hivyo, ukosefu wa mtaji huwa kikwazo kikubwa. Hali ya kiuchumi na masharti magumu ya mikopo pia huwazuia vijana wengi kufanikisha ndoto zao za ujasiriamali.  Kwa mfano, wanafunzi wengi huwa na dhana ya kupata ajira mara baada ya kuhitimu elimu ya juu lakini wanajikuta katika dimbwi la wahitimu wasio na ajira hivyo kujiunga na biashara. Isivyo bahatizbiaahara hizo nazo huwa na changamoto ya mtaji wa kuanzisha ama kuendeleza biashara hiyo.   CHANGAMOTO ZA KIAKILI NA KIHISIA Changamoto za kiakili na kihisia ni tatizo linalowakumba vijana wengi wanaotoka vyuoni, hasa wanapokutana na hali halisi ya maisha ambayo mara nyingi haitoshelezi matarajio yao. Baada ya miaka ya kujituma masomoni, kukosa ajira au kukabiliana na presha za familia na jamii huwafanya vijana wengi kuhisi mfadhaiko, wasiwasi, na hata msongo wa mawazo. Aidha, ukosefu wa uzoefu wa kukabiliana na changamoto za kifedha, mahusiano, na maisha ya kujitegemea huongeza mzigo wa kihisia. Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili kama vile huzuni ya kudumu na kupoteza hamu ya kuendelea na juhudi za kujenga maisha yao. Ili kukabiliana na hali hii, vijana wanapaswa kupata msaada wa kisaikolojia, elimu ya kiakili, na kuungwa mkono na familia pamoja na jamii.   HITIMISHO NA MAPENDEKEZO Changamoto hizi zinahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa serikali, mashirika binafsi, na jamii kwa ujumla. Serikali inaweza kuweka mikakati ya kukuza ajira, kuboresha mitaala ya elimu ili kuendana na mahitaji ya soko, na kutoa ruzuku kwa wajasiriamali vijana. Vilevile, vijana wanapaswa kuwa wabunifu na kutafuta njia mbadala za kujiajiri na kujifunza ujuzi wa ziada. Kwa kushirikiana, tunaweza kuhakikisha kuwa wahitimu wa vyuo wanapata fursa ya kutumia maarifa yao kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na jamii kwa ujumla.

CHANGAMOTO ZA VIJANA WANAOTOKA CHUO NA KUKABILIANA NA MAISHA MTAANI. Read Post »

kasuku mbstrinitycare

Kasuku! Raha sana!

By Nasibu Mahinya Tofauti na viumbe wengine, kasuku anaongoza kwa kufugwa na watu katika makazi yao. Kwa miaka mingi, ndege kasuku amekuwa kivutio kwa binadamu  kutokana na sifa zake za kipekee. Miaka hivi ya karibuni, tafiti zimegundua kuwa jumla ya idadi ya ndege millioni 14 wanaishi kama mateka nchini Marekani na ndege hao wanasemekana kutoka mabara tofauti na zaidi ya asilimia hamsini ya ndege hao ni kasuku. Kasuku yupo tofauti na viumbe wengine kwa sababu ndege huyu huishi miaka mingi na ana uwezo mkubwa wa akili. Hivyo basi makala hii itakusaidia kumjua zaidi iwapo kama hukupata nafasi ya kumjua kipindi wengi wakiwa wanamfuga ndege huyu mpiga domo. Uzuri ni kwamba, Kasuku hachagui sana msosi, anakula karibu kila kitu. Kuna aina nyingi za kasuku Kuna aina takribani 350 za kasuku duniani wenye rangi za tofauti za kuvutia kama buluu, njano, kijani, nyeupe, nyeusi na nyekundu. Barani Afrika, kasuku wa kijivu ndiyo hupatikana kwa wingi zaidi. Kasuku wengi hutekwa Robo tatu ya kasuku wote duniani wapo kwenye hatari ya kupotea kwenye uso wa dunia kwa sababu ya shughuli za binadamu za ukataji miti na biashara haramu ya kusafirisha na kuuza wanyama.  Jike au dume? Ni ngumu sana kutofautisha kasuku dume na jike, Wanafanana asilimia 99.9. Watu wengi zamani walikuwa wananunua kasuku mtaani alafu wanajikuta wana madume mawili yanatazamana humo bandani. Mdomo wa ajabu kidogo Kasuku ana mdomo uliyojikunja kuelekea chini kama mundu na anakula chochote anachokutana nacho kuanzia nyasi, matunda, mbegu, majani, maua mpaka nyama. Kasuku ana ulimi ambao hautumii kuonja chakula, kazi ya kuonja chakula hufanywa na upande wa juu wa ndani ya mdomo. Kasuku hata siyo mzito Kulingana na aina ya kasuku, ndege huyu anaweza kuwa na uzito wa kuanzia gramu 60 mpaka kilo moja na nusu. Kasuku anakula chumvi nyingi! Kasuku anaweza kuishi hadi miaka hamsini, na kasuku mzee kuliko wote ana miaka 86 na anaishi kwenye hifadhi iitwayo Brookfield iliyopo mjini Chicago, nchini Marekani. Kuna watu walifuga kasuku wakaacha migogoro ya mirathi, familia haikujua nani atamrithi huyo ndege. Ya Mungu mengi na miaka 50 ni mingi kweli kweli. Kasuku ana kinga asilia Manyoya ya kasuku yana kinga dhidi ya bakteria. Kinga ambayo huwapa manyoya yao rangi nyekundu, kijani na njano. Hachelewi kuhama kambi Kasuku huhama pale hali ya hewa inapobadilika kutafuta malisho. Hata kama nyumbani kwako kuna vitu asivyovipenda, usishangae siku moja hujafunga banda vizuri, anaondoka na hutomuona tena. Kasuku anapiga domo! Kasuku anapenda sana kupiga domo. Yeye hana uwezo wa kuongea bali ana uwezo wa kukariri maneno yanayosemwa na mwanadamu, hivyo basi kuwa mwangalifu na maneno uyasemayo mbele ya kasuku maana atayarudia tu muda wowote. Kasuku anayeshikilia rekodi ya dunia ya kujua maneno mengi alikariri maneno 1,700. Ingawa hatuwezi tena kumfuga mjumbani lakini pata picha kasuku kakaririshwa nyimbo afu kapelekwa kuimba kwenye ‘karaoke Raha’ sana!

Kasuku! Raha sana! Read Post »

Afya ya akili na mbstrinitycare

MSAADA WA KITAALAMU JUU YA AFYA YA AKILI

By Sylvia Mtenga Hapa kuna orodha ya vitabu kumi vinavyoweza kumsaidia mtu kuelewa zaidi kuhusu afya ya akili na jinsi ya kushughulikia changamoto za kiakili katika maisha ya kila siku. Vitabu hivi vimeandikwa na wataalamu wa saikolojia, wanasaikolojia, na watu wengine wenye uzoefu katika nyanja ya afya ya akili: 1. The Body Keeps the Score na Bessel van der Kolk Kitabu hiki kinachambua jinsi mwili unavyohifadhi kumbukumbu za kiwewe (trauma) na athari zake kwenye afya ya akili na mwili. Bessel van der Kolk anaelezea kwa kina jinsi watu wanaweza kuponya majeraha ya kiwewe kupitia mbinu kama tiba ya mwili, tiba ya akili, na mbinu nyingine za kitiba. 2. Lost Connections na Johann Hari Katika kitabu hiki, Johann Hari anaangazia sababu za msongo wa mawazo na unyogovu, akichambua jinsi watu wanavyoweza kupata furaha ya kweli kupitia mawasiliano mazuri na jamii. Hari anasisitiza umuhimu wa kujumuika na watu wengine kama sehemu ya kuimarisha afya ya akili. 3. Man’s Search for Meaning na Viktor E. Frankl Kitabu hiki ni hadithi ya kihisia ya Viktor Frankl, ambaye alinusurika kambi za mateso za Nazi na baadaye kuunda mbinu ya Logotherapy. Frankl anaelezea jinsi kutafuta maana maishani kunaweza kusaidia watu kukabiliana na changamoto kubwa za kiakili. 4. Feeling Good: The New Mood Therapy na David D. Burns Kitabu hiki ni mwongozo wa kuepuka mawazo hasi, kwa kutumia mbinu za tiba ya utambuzi (Cognitive Behavioral Therapy – CBT). David D. Burns anatoa mbinu za kushughulikia unyogovu na kuongeza furaha maishani kwa kubadilisha mitazamo na mawazo. 5. The Happiness Trap na Russ Harris Russ Harris anaelezea jinsi mbinu za Acceptance and Commitment Therapy (ACT) zinavyoweza kuwasaidia watu kushinda wasiwasi na unyogovu. Kitabu hiki kinatoa mbinu za kukubaliana na changamoto badala ya kupambana nazo. 6. Daring Greatly na Brené Brown Kitabu hiki kinachunguza jinsi aibu, hofu, na kukosa uthubutu kunavyoweza kuathiri maisha yetu. Brené Brown anaonyesha jinsi watu wanavyoweza kukubali udhaifu wao na kuishi maisha ya ujasiri na utimilifu, jambo muhimu kwa afya ya akili. 7. Mindfulness in Plain English na Bhante Henepola Gunaratana Kitabu hiki kinaelezea kwa undani mbinu za uangalifu (mindfulness) na jinsi zinavyoweza kuleta amani na utulivu. Bhante Henepola Gunaratana anafafanua jinsi uangalifu unaweza kusaidia watu kuondoa wasiwasi na mawazo hasi. 8. An Unquiet Mind na Kay Redfield Jamison Kitabu hiki ni simulizi la maisha ya Kay Redfield Jamison, profesa wa saikolojia anayesumbuliwa na matatizo ya hisia. Ni ushuhuda wa kweli wa jinsi matatizo ya afya ya akili yanaweza kuathiri maisha na jinsi ya kukabiliana nayo. 9. The Power of Now na Eckhart Tolle Eckhart Tolle anafundisha jinsi ya kuishi wakati wa sasa kunaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na hofu. Kitabu hiki kinawahamasisha wasomaji kuzingatia wakati wa sasa kama njia ya kukuza afya ya akili na utulivu wa ndani. 10. Emotional Intelligence na Daniel Goleman Daniel Goleman anachunguza umuhimu wa akili ya kihemko na jinsi inavyoweza kuchangia ustawi wa kiakili na mafanikio maishani. Kitabu hiki kinatoa mbinu za kudhibiti hisia na kuboresha uhusiano wa kijamii. Vitabu hivi vinatoa mwanga katika nyanja tofauti za afya ya akili na vinaweza kuwa msaada mkubwa kwa mtu yeyote anayejitahidi kuelewa, kudhibiti, na kuimarisha afya yake ya kiakili.

MSAADA WA KITAALAMU JUU YA AFYA YA AKILI Read Post »

Migogoro juu ya Mirathi mbstrinitycare

DISPUTES OVER INHERITANCE.

By Jamal Hamza  Cordoba Law Firm defined inheritance dispute as a situation where a decedent’s beneficiaries or family members are in disagreement about how the decedent’s estate should be divided. Dispute arises when conflicts or disagreements occur over how a deceased person’s assets are divided. These conflicts can be triggered by several factors, such as questioning the validity of a will or differing views on how the assets should be distributed among the heirs. Such disputes are often complex and emotionally charged, typically involving family members with various expectations and needs.  (T. Tezzer,2005). Also, different interpretations of the will, challenges to its legality, disagreements over how to divide or value assets, or concerns related to the legally mandated portion of the estate that must be left to specific individuals, such as a spouse or children. In such cases, resolving the matter may involve legal proceedings, mediation, or arbitration to reach an agreement on how the inheritance should be divided. In Tanzania, inheritance laws are governed by a combination of statutory law, customary law, and religious law depending on the circumstances and the background of the deceased. Let us look up on these laws, ambiguity and blended family as a cause family disputes over inheritance. Statutory Law: According to Tanzania Human Right Jurisprudence statutory law are laws passed by local legislature. This law outline procedures for the administration of both testate and intestate estates. To a testate estate in Tanzania, if the deceased has left a valid will, the estate is distributed according to the term of the will. If the deceased did not leave a will the distribution of estate fall to the spouse, children, parents, and other close relative entitle to inherit in specific shares outlined by law. The disputes come to arise when the statutory law mix up with customary law, Islamic law or when it does not align with the expectation of the family members. For example, sons may expect to inherit the bulk of the estate according to the customs but statutory law may require equal distribution among all children leading to family conflicts. 2. Customary law: It is applied when the deceased lived according to the customs and traditions of their tribe. Customary law will only be used if the individuals involved in the inheritance belong to the same tribe, and not otherwise. According to (T. Tezzer 2005), in this system, the eldest male child from the primary household receives the largest portion of the estate, followed by the other male children, while the female children from any household receive the smallest portion (T. Tezzer,2005). These customary practices can lead to significant challenges and conflicts among family members. Many modern communities strongly oppose such customs and traditions, which results in conflicts between those who follow their traditional customs and those who do not.   3. Islamic law: It is applied to followers of the Islamic faith. The distribution of the deceased’s estate according to Islamic law. The main heirs in Islamic law are the wife or wives, father, mother, and children. According to Tamar Tezzer, Islamic law facially discriminate against widows and daughters, granting women half of the share of men, (T. Tezzer,2005). The eldest male child from the primary household receives the largest portion of the estate, followed by the other male children, while the female children from any household receive a smaller portion. A child born out of wedlock does not have the right to inherit unless there is a will. Such religious laws can sometimes lead to conflicts, as some people view them as discriminatory and accompanied with nepotism. 4. Blended families Often blended families have impact to inheritance disputes due to the complex relationships between children, stepchildren, spouses, and ex-spouses. (T. Tezzer,2005).   Children from a previous marriage may feel that their biological parent is favouring their new spouse or stepchildren when dividing assets. They might believe they are entitled to a larger portion of the estate, especially if they had a closer relationship with the deceased.  In cases where the deceased has not left a clear will, conflicts arise over how assets should be distributed. Children from previous relationships may worry that their inheritance will go to the surviving spouse or stepchildren. 5.  Ambiguity Ambinguity in a will can lead to serious family disputes over inheritance because unclear or vague language can result in different interpretations of the deceased’s intentions. If a will lacks specificity, family members may argue over who gets what. (T. Tezzer,2005).  For example, if a will states, “I leave my property to my children,” without specifying which property or how it should be divided, siblings may fight over who is entitled to more valuable assets, such as a family home or a business. Ambiguous phrases like “my favourite child” or “my close friend” can create confusion. For example, if the will says, “I leave a portion of my estate to my favourite nephew,” but the deceased had several nephews, each may claim they are the intended beneficiary, sparking disputes over who should receive that share.  If the will hasn’t been updated after significant life events such as divorce, remarriage, or the birth of new children, disputes can occur. For example, if the deceased left assets to a former spouse or failed to mention new stepchildren, both biological and stepchildren might dispute who is the rightful heir, especially in blended families.

DISPUTES OVER INHERITANCE. Read Post »

Thanks Giving mbstrinitycare

THANKSGIVING

by: Justin Mwita “Thanksgiving gives us an incredible opportunity to practice real gratitude, drop our burdens, and remind ourselves we have a Heavenly Father willing to handle it.” Be anxious for nothing, but in everything by prayer and supplication, with thanksgiving, let your requests be made known to God. Thanksgiving is an opportunity to realign our hearts with gratitude. It offers a remedy for anxiety: prayer and thanksgiving. Even in chaos, gratitude unlocks God’s peace in our hearts, reminding us it’s not just a response to blessings but a way to trust His faithfulness. The Pilgrims’ story in 1621 shows the power of gratitude during hardship. Despite severe losses, they celebrated God’s provision with thanksgiving. Their faith, not abundance, sustained them. Similarly, rusting God’s care brings calmness like a child with its mother. In today’s world of abundance, we often overlook gratitude, leading to dissatisfaction. Paul’s advice to “be anxious for nothing” is challenging, but prayer with thanksgiving shifts our focus from lack to God’s provision, inviting His peace. Cultivating gratitude daily can help: Start with thanks: Name three things you’re grateful for each morning, no matter how simple. Reflect on God’s faithfulness:  Recall past blessings to fuel trust for the future. Pray with gratitude: Thank God for His goodness before presenting requests. Share gratitude: Encourage others by sharing your blessings. Gratitude transforms anxiety into peace, peace for it is said that God’s peace will guard you hearts and minds. Trusting God allows us to release burdens and rest in His care. This Thanksgiving, go beyond traditions and practice gratitude daily. Reflect on your blessings, pray over them, and share them with others. Gratitude opens our hearts to God’s peace, even in hard times. REFLECTION Reflect on the blessings in your life, especially those that may have come through difficult seasons. Consider how God has been faithful in providing for you and guiding you. Take a moment to recount specific ways He has shown His love and care, even when circumstances were challenging. Allow these reflections to remind you of His unchanging faithfulness. Start each day by naming three things you’re thankful for and let those moments of gratitude shape your attitude and perspective. As you pray, focus on thanking God for His goodness before bringing your requests to Him. Trust that as you cultivate gratitude, His peace will guard your heart and mind, bringing you comfort and hope.

THANKSGIVING Read Post »

Alizeti ni ua au zao mbstrinitycare

Zao la Alizeti: Utalii, kilimo vinapokutana pamoja.

By Nasibu Mahinya Wanasema bustani haikamiliki bila maua na huo ni ukweli usiopingika, maua huongeza mvuto na maua mengine yana tija kwenye lishe yetu pia.  Napenda nikujuze kuwa zaidi ya asilimia 99 ya matunda yote duniani hutokana na maua. Moja ya vigezo vyangu vya kutafuta mke wa kuoa ni kuwa mwanamke lazima apende na ajue jinsi ya kuhudumia bustani ya maua, tena akiweka na maua ya alizeti atanifurahisha sana. Je, Alizeti ni ua? Lina upekee gani katika sekta ya kilimo na utalii? Twende pamoja. Asili ya ua la alizeti ni kaskazini mwa Amerika na lilikuwa likiota kama ua pori huku likitoa bidhaa kama dawa na mafuta hadi kuanza kulimwa kibiashara miaka ya 1500 na wazungu waliolowea Marekani na mwishowe ua hilo kusambaa duniani kote. Ua hili lenye muundo wa kisahani, lina rangi ya njano kwenye petali na kahawia iliyokolea katikati kwenye mbegu. Ua hili kwa Kiingereza linaitwa ‘Sunflower’ na ni kutokana na sura yake kufanania muonekano wa jua. Lakini pia kwa kifaransa linaitwa ‘Tournesol’ ikimaanisha ‘kugeukia jua’ ambayo ni sifa nyingine ya ua hili. Ua hili lina uwezo wa kugeukia upande ambao mionzi ya jua hutokea. Sifa kuu za alizeti Mmea wa alizeti unaweza kuwa na urefu wa hadi futi 12, sawa urefu wa watu wawili kwenda juu. Alizeti refu kuliko duniani lilikuwa na urefu wa futi 30, lilioteshwa nchini Ujerumani. Katikati ya ua la alizeti kuna mbegu zisizopungua elfu moja, mbegu hizo ambazo zikikamuliwa hutoa mafuta ya kupikia ya alizeti yenye vitamin A na D na yasiyo na lehemu, yani Kolestro. Kazi ya alizeti katika shughuli mbalimbali Alizeti ambalo limeshavunwa mbegu linaweza kutumika kama dodoki la kujisugulia mwili wakati wa kuoga. Alizeti pia hufanya kazi nzuri ya kunyonya miyonzi ya sumu iliyomo kwenye hewa na kwenye udongo. Kwa mfano, nchini Japan zaidi ya mimea ya alizeti ilipandwa ili kupambana na mionzi ya nyuklia baada ya Tsunami kubomoa matenki ya uranium kwenye kitongoji cha Fukushima mwaka 2011. Alizeti linavutia sana nyuki hivyo kama mfugaji wa nyuki akipanda maua haya yanaweza kumuongezea faida katika mavuno yake ya asali. Alizeti ni zao linalovutia watalii Maua ya alizeti ni kivutio cha watalii hasa wanaopenda kupiga picha zenye maua yanayovutia. Barani Afrika, zao la alizeti lililetwa na wakoloni na Tanzania ni moja ya nchi 10 duniani zinazoongoza kwa uzalishaji wa zao hili ambapo zaidi ya tani laki tatu huvunwa kila mwaka.  Katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Singida na Kilimanjaro ni baadhi ya sehemu ambazo maua haya hupatikana kwa wingi, lakini je, alizeti na muonekano wake wa kuvutia linaishia tu kuwa zao la kibiashara alafu basi? Nchi kama Marekani na Ukreini ni moja kati ya nchi za kwanza zilizoona fursa ya utalii ndani ya ua la alizeti.  Kwa kuwa maua haya yanavutia machoni na watu wakipiga nayo picha hupendeza, basi mataifa hayo yamebuni aina ya utalii uitwao utalii wa kilimo yaani ‘Agritourism’ ambao unahusisha watalii kutembelea mashamba yakiwemo ya alizeti, kujionea jinsi kilimo hicho kinavyofanywa na pia kupiga picha ambazo zitabakia kuwa kumbukumbu za kudumu milele. Utalii wa alizeti pia huangukia kwenye utalii wa maua kama ambao yaliyopo kwenye hifadhi ya Taifa ya Kitulo japokuwa maua ya hifadhi hiyo ni uoto wa asili. Je, wewe ni mkulima wa alizeti na ungependa kupata watalii watakaolipia ziara za shambani kwako? Fursa iko wazi hiyo!

Zao la Alizeti: Utalii, kilimo vinapokutana pamoja. Read Post »

Migogoro ya nafsi mbstrinitycare

KUTATUA MIGOGORO YA NDANI NA NAMNA YA KUJIBORESHA

By Sylvia Mtenga 1. Utangulizi Migogoro ya ndani ni hali zinazotokea pale ambapo mtu binafsi anakumbana na changamoto zinazotokana na hisia, mawazo, na matendo yake mwenyewe. Migogoro hii inaweza kujumuisha hisia kama wasiwasi, hofu, chuki, na hata kutoridhika kwa ujumla. Migogoro ya ndani inaweza kusababisha madhara makubwa endapo haitashughulikiwa kwa wakati, ikiwemo athari kwenye afya ya akili, uhusiano na hata uwezo wa kufikia malengo. Kujiboresha ni mchakato wa kudumu wa kujijenga, kujifunza na kuboresha utu na uwezo binafsi. 2. Sababu za Migogoro ya Ndani Migogoro ya ndani inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwemo: 3. Mbinu za Kutatua Migogoro ya Ndani a) Kutafakari na Kujitathmini Kutafakari inasaidia mtu kuweza kuangalia kwa undani mawazo na hisia zake, kutambua chanzo cha migogoro hiyo, na kujua njia sahihi za kuiangalia kwa mtazamo chanya. b) Kujenga Imani na Kujiamini Kujenga imani kwa mtu mwenyewe ni hatua muhimu sana katika kutatua migogoro ya ndani. Mtu anapaswa kujikubali jinsi alivyo na kujifunza kuthamini uwezo na nguvu zake binafsi. c) Kupanga Malengo Yanayowezekana Kufikiwa Kupanga malengo madogo na yanayoweza kufikiwa ni muhimu kwa sababu huwasaidia watu kupata motisha na kuepuka hisia za kushindwa. Kwa kufanya hivyo, mtu anaweza kushinda changamoto ndogo moja baada ya nyingine. d) Kutafuta Msaada wa Kitaalamu Wakati mwingine, migogoro ya ndani inaweza kuwa ngumu kutatuliwa bila msaada wa nje. Wataalamu wa afya ya akili, kama vile wanasaikolojia, wanaweza kutoa mwongozo na mbinu maalum za kutatua migogoro. e) Kubadilisha Mtazamo Kubadilisha mtazamo kutoka hasi kwenda chanya ni njia bora ya kutatua migogoro ya ndani. Hii inahusisha kujifunza kuangalia mambo kwa upande bora na kuthamini mambo madogo ambayo mtu amefanikiwa. 4. Namna ya Kujiboresha a) Kusoma na Kujifunza Kusoma vitabu na kujifunza kupitia makala, video na kozi mbalimbali kunaweza kumsaidia mtu kupata maarifa na mbinu mpya za maisha. b) Kuunda Tabia na Mazoea Chanya Mazoea kama kufanya mazoezi ya mwili, kula vyakula vya afya, na kujenga ratiba bora ya usingizi ni muhimu katika kujiboresha kimwili na kiakili. Mazoea haya humsaidia mtu kuwa na nguvu na afya bora, pamoja na kuwa na hali nzuri ya kimawazo. c) Kushirikiana na Watu Wenye Mitazamo Chanya Kuwepo karibu na watu wanaokuunga mkono, wenye malengo kama yako, na wenye mitazamo chanya husaidia kukuza moyo wa kuendelea mbele. d) Kujifunza kutoka kwa Makosa Kujiboresha kunahitaji mtu kuwa tayari kujifunza kutokana na makosa. Kwa kutambua makosa yaliyopita, mtu anaweza kujua mambo ya kuepuka au kuboresha katika hatua zake zijazo. e) Kujenga Nidhamu na Kujitolea Nidhamu ni kipengele muhimu sana katika kujiboresha. Kwa kujitolea na kuwa na nidhamu katika shughuli za kujijenga, mtu anaweza kufikia malengo yake na kuboresha maisha yake kwa ujumla. 5. Hivyo basi, Kutatua migogoro ya ndani na kujiboresha ni mchakato unaoendelea na unaohitaji mtu kuwa na uvumilivu, kujikubali, na mtazamo chanya. Kwa kutumia mbinu sahihi, kila mtu anaweza kujenga maisha yenye afya bora ya kiakili na kimwili, na hivyo kujenga msingi wa maisha yenye furaha na mafanikio.

KUTATUA MIGOGORO YA NDANI NA NAMNA YA KUJIBORESHA Read Post »

Scroll to Top